Uchunguzi : Wakati Serikali ikikuza sekta ya viwanda ili kupunguza tatizo la ajira nchini, ukuaji wa sekta hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa ajira za muda na za kudumu. Ajira hizi zimekuwa hazina ubaguzi wa jinsi kwa jicho la nje, japo kwa jicho la ndani yapo mengi yanayoendelea...