SALA YA SHEDRACK,MESHAKI NA ABEDNEGO.
Utukuzwe na kusifiwa,ee Bwana,Mungu wa babu zetu! Jina lako litukuzwe milele,yote uyafanyayo,wayafanya kwa haki kabisa,matendo yako yote ni mema,na njia zako ni sawa,na hukumu zako zote ni za haki.
Katika mambo yote sisi tumekukosea sana, wala hatukuzitii...