KUACHA KAZI
Baada ya kutoka Burma, siku moja, Utubora alisimama katika ofisi mbele ya tajiri wake kumwambia kuwa alitaka kuacha kazi. Kazi yake ilikuwa ukarani katika ofisi kubwa ya biashara ya karafuu. Mshahara wa Utubora ulikuwa simulizi karibu katika Unguja nzima; ilisemwa pia kuwa uliwatia...