Bunge lilipitisha sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi na kupitisha kuwa kutakuwa na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
Mbona mpaka leo bado wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ndiyo bado wako ofisini na wanaendelea na majukumu kama kawaida licha ya Sheria ya Tume Huru Kupitishwa na Bunge.
Naomba...
Nawaombeni sana mnieleweshe kuhusu TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI na TUME HURU YA UCHAGUZI.
Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatamka kuwa kutakuwa na TUME YA TAIFA UCHAGUZI na Sheria ya 2024 inatamka kuwa kutakuwa na TUME HURU YA UCHAGUZI. Je, ni kipi kiheshimiwe kwanza. Ni Katiba au Sheria?
Sheria hii inabainisha muundo, majukumu, utaratibu wa upatikanaji wa Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na sifa za Mkurugenzi wa Uchaguzi, kuweka utaratibu wa uendeshaji wa vikao vya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuweka masuala mengine yanayohusiana na hayo.
Kwa mujibu wa Sheria hii...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.