Maji huku Mwanza imekuwa ni kero kubwa sana, wanachuo tunaishi kwa tabu sana tunapata shida kubwa ya maji ilihal tuko karibu na ziwa Victoria
Sijui mnatusaidiaje kuepukana na hili. Tunalipia bili za maji kwa wakati lakini bado maji kuyapata ni changamoto.
Ni siku ya 4 sasa maji hayatoki
Malimbe asilimia kubwa ya wakazi ni wanafunzi wa chuo cha SAUT kwa asilimia 75 haichukui zaidi ya KM 10 kwa mkazi yeyote wa malimbe kufikia ziwa victoria lakini changamoto ya maji ni kubwa sana inafikia zaidi ya siku 4 mpaka 5 maji hayatoki.
Tunaoba mlifanyie kazi hili tunaishi kwa taabu sana.
Wakazi wa mwanza, wilaya ya nyamagana kata ya Buhongwa maji yamekuwa ni changamoto sana, tuna wiki ya pili hatuna maji na kila mara hii hali hujirudia rudia.
Tushalifikisha mpaka kwa mwenyekiti lakini jambo limekuwa kizungumkuti.
Hii changamoto utatatuliwa lini?
Pia soma
KERO - Tatizo sugu...
Anonymous
Thread
maji nyamagana
shidayamajimwanza
usugu wa maji buhongwa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.