Asubuhi ya leo Januari 14, 2025 pameamka na sintofahamu baina ya Daniel Naftali ambaye ni Meneja wa Kampeni(Campaign Manager) wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akizozana na aliyekuwa Mgombea wa Uenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA)
Taifa Shija Shibeshi
Inaelezwa kuwa...
Kijana Shija Shibeshi, aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, ametangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
Shija ameomba wafuasi wake kumuunga mkono Wakili Deogratias Mahinyila, ambaye ameeleza kumuunga mkono Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.