Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, ametoa wito kwa viongozi na wanasiasa wa mkoa huo kufanya siasa za kistaarabu badala ya siasa za chuki na zinazogawa wananchi akisema hazitavumiliwa mkoani humo.
Kanali Mtambi ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa...