Silasi Ndosi (38) mkazi wa Shangarai wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha amekutwa amefariki dunia, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya mikwaruzo sehemu za kifuani na mgongoni.
Mbali na mikwaruzo pia mwili huo ulikutwa ukitoka damu puani, masikio, na mdomoni.
Akizungumza leo Novemba 14, 2024...