NAMTAKA SINGO MAZA
1 Nimehangaika sana, kuyatafuta mapenzi
Niliowapa amana, hata hawakuienzi
Nikapigwa dana dana, na kufanyiwa ushenzi
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
2 Aloumizwa ja mimi, huenda tukalandana
Hatusikizi akwami, wawili tukipendana
Tukuze wetu uchumi, mawazo kuliwazana...