Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas,amemsifu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dk Damas Ndumbaro kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo katika jimbo hilo.
Kanali Abbas ametoa kauli hiyo mbele ya wananchi wa Kata ya Subira, Manispaa ya Songea...