Baada ya miaka 16 ya kutembea kilomita 40 kutafuta huduma za afya, wananchi wa vijiji vitatu wilayani Tandahimba mkoani Mtwara hatimaye wamepata suluhisho.
Kituo cha Afya cha Maheha kilichogharimu shilingi milioni 400 sasa kimeanza kutoa huduma na wananchi wengi hususan wanawake wamejitokeza...