Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.
Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki...