Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa zinazoweza kuleta madhara zinatarajiwa kunyesha katika mikoa 11 ya Tanzania.
Mikoa hiyo ni Ruvuma, Njombe, Iringa, Morogoro, Mbeya, Songwe, Rukwa, Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara.
Katika taarifa iliyotolewa leo Desemba 27, 2022 na TMA...