Wadau hamjamboni nyote?
Haijataja kutokea kwenye historia ya mapikezi ya timu ya soka Tanzania
Maelfu Kwa maelfu ya wapenzi wakesha usiku wakisubiri kuwasili kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania.
Kule Afrika Kusini Yanga imecheza na Kaizer Chiefs kombe la TOYOTA na kulazimika kuvaa logo ya TOYOTA kifuani mwa jezi yenye rangi nyekundu. Binafsi nilidhani Yanga inakataa logo za wadhamini zenye rangi nyekundu kwa kuhofia kupata mikosi ya kufungwa kumbe bwana hakuna kitu hicho ni hofu tu...
Timu ya Yanga kesho itatupa karata ya pili katika mashindano ya Mpumalanga cup kwa kucheza dhidi ya TX Galaxy.
Mechi itakuwa live Azam sport 1 HD saa kumi jioni. Mechi ya Yanga ya kesho itahitimisha mashindano ya Mpumalanga kisha itahamia kwenye mashindano ya Toyota Cup tarehe 28 kwa kukipiga...