tuma kwa namba hii

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. Mr Why

    TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja tu Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA

    TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA TCRA chukueni ushauri wangu mtateketeza matapeli wote ndani ya miezi mitatu Swala la utapeli wa meseji za tuma kwenye namba hii ni kama limewazidi akili...
  2. Waufukweni

    TCRA: Matapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" tumewapunguza

    Vitendo vilivyoripotiwa vya ulaghai kwenye mitandao ya simu vimepungua kwa asilimia 28 kati ya Juni na Septemba mwaka huu, kutokana na hatua kali za serikali na kampeni za kuongeza uelewa wa watumiaji. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt Jabiri Bakari, alifichua...
  3. Mtoa Taarifa

    TCRA: Utapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" umepungua sana nchini

    Akizungumza kupitia Power Breakfasta leo Oktoba 30, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa laini za simu tofauti ipo kubwa sana. Ukiangalia ripoti ya Robo mwaka ya performance ya mawasiliano kwenye takwimu za mawasiliano...
  4. gcmmedia

    Ukitumiwa ujumbe na Matapeli huwa unajibu nini?

    Ukitumiwa ujumbe mfupi na matapeli wa mtandao wale ambao wanaandika “tuma ile pesa kwenye namba ” Huwa unajibu nini? Na unachukua hatua gani?
  5. FRANCIS DA DON

    ‘Tuma kwa namba hii’ wapatiwa muarubaini, mwisho wao umefika

    Napendekeza kanuni mpya! Kanuni mpya ni kwamba, NIDA moja hairuhusiwi kusajili zaidi ya namba moja kwa mwezi. Sasa mtu NIDA yake ikitumika kufsnys utapeli kwa laini iliyosajiliwa baada ya kuanza kanuni hii mpya atatueleza, wakala alimsajilisha vipi namba ya ziada? Maana yake mwenye NIDA ndio...
  6. Zegota

    Hii Issue ya Utapeli wa "Tuma Kwa namba hii" nadhani wafanyakazi wa makampuni ya simu wanahusuka Kwa asilimia kubwa

    Habari zenu wakuu. Mzee Ayo huko Arumeru amemaliza safari yake ya hapa Duniani, ni chanzo kikitajwa ni utapeli wa mtandaoni maarufu " Tuma Kwa namba hii" Kwenye hili tuache unafikia hawa watu wa mitandao ya simu inawezekana wapo wengi sio waaminifu na wao ndio wanaoinjinia huu utapeli . Natoa...
  7. Satirical Yet Awesome

    Tuwe makini, nahisi hii mitandao ya simu haina ulinzi wa uhakika

    Iko hivi, siku za nyuma kama wiki tatu zilizopita nilikuwa naongea na mama kweny simu, tulikuwa tunaongea kuhusu maswala ya kutumiana pesa, nikwambia ntamtumia muda si mrefu tukimaliza kuongea, cha kushangaza baada ya kukata tuu simu, kuna message ikaingia ya namba nyingine ngeni inasema...
  8. Hismastersvoice

    TCRA tunahitaji jibu kwenye huu uhalifu wa 'tuma kwa namba hii'

    Tunapata ujumbe au simu kutoka kwa watu wanaotumia baadhi ya mitandao ya simu, ujumbe maarufu ni wa "ile pesa tuma kwenye namba hii", tukiacha ujumbe kuna wanaotupigia simu wakijidai ni wafanyakazi wa kampuni ya simu ambao wanakuuliza kuhusu pesa zilizotumwa kwenye akaunti yangu, hawa huishia...
  9. Roving Journalist

    Kisutu: Matapeli 12 wanaotuma Meseji za kitapeli kwenye simu, Wapandishwa Kizimbani

    "MIMI MWENYE NYUMBA WAKO APA MBONA SIKU ZINAZIDI?" 12 WAFIKISHWA MAHAKAMANI, WAKABILIWA MASHTAKA 32. Na. Jeshi la Polisi, Dar es Salaam, Mei 28, 2024 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani wakazi 12 wa Ifakara, Morogoro akiwemo Barnaba Gidajuri (45) wakikabiliwa na mashtaka...
  10. GENTAMYCINE

    85% ya Wezi / Matapeli wa Mitandaoni ( Tuma kwa Namba hii ) wanatokea / wako Ifakara Mkoani Morogoro

    "Huwa wanakaa katika Nyumba Moja huku Wake zao wakiwa busy kuwapelekea Vyakula. Na baadhi yao ni Wasomi wakubwa sana tu hadi wana Doctorates ( PhD ) zao" Nukuu hii nimeitoa EFM Radio Asubuhi hii baada ya kumsikia Bwana Innocent Mungi Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Habari na...
  11. P

    Tuma kwa namba hii wamewatoa knock-out mpaka sasa, mmeona la msingi ni kuzuia VPN?

    Wakuu, Inasikitisha sana na kutia uchungu kuwa na Waziri mzigo kwenye wizara muhimu kama hii. Badala ya kuwa vinara wa kutetea uhuru wa maoni na kukinda taarifa binafsi na faragha za wananchi wenyewe ndio wanakuwa wa kwanza kuminya uhuru wa maoni, kuingilia faragha za watu na kutunga sheria...
  12. benzemah

    Polisi Tanga yanasa watu 11 wakidaiwa ni "Tuma kwa namba hii"

    Tanga. Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga likiwashikilia watuhumiwa 11 kwa makosa ya utapeli kwa njia ya mandao, majirani katika nyumba waliyokuwa wakiishi watuhumiwa hao wamesema wakiwa humo walikuwa na utamaduni wa kufungua muziki kwa sauti kubwa. Pia wanadai watuhumiwa waliokuwa wamepanga...
  13. Heparin

    Unazungumziaje hali ya Utapeli unaofanyika kwa njia ya Simu baada ya kuzimwa kwa laini zisizohakikiwa?

    Kwa mujibu wa ripoti ya TCRA ya robo ya nne ya mwaka, hadi Desemba 2022 mitandao ya simu nchini ilikuwa imesajili jumla ya laini milioni 60.277. Laini hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na zile milioni 58.1 waliokuwapo mwisho war obo ya tatu ya mwaka 2022 yaani Septemba...
  14. BARD AI

    11 mbaroni wakituhumiwa kutapeli kwa ujumbe wa ‘Tuma kwa namba hii’

    Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 11 Kwa tuhuma za utapeli kwa njia ya mitandao. Watuhumiwa hao ni wale ambao wanadaiwa hutuma ujumbe mfupi Kwa njia ya simu, 'Ile pesa tuma kwa namba hii', ambapo wamekamatwa na simu za kiganjani 19 pamoja na fedha Sh700,000 ambazo wanadaiwa...
  15. Kakijana

    Utapeli wa mitandao, usumbufu wa "Tuma kwenye namba hii"

    Wakuu poleni na majukumu. Hoja ninaipeleka kama "mkopo", maana leo ni "freeday" ya karibu kabisa na ATM za sikukuu za mwisho wa mwaka. Kuna kale kaujumbe kanaingia paaap! na unakumbuka jana "rafiki mpya" kwaajili ya sikukuu kakutajia namba moja kati ya mbili ulizo na uhakika nazo kuwa ana...
  16. The Sheriff

    KERO TCRA, hawa matapeli wa “TUMA KWA NAMBA HII” tutaishi nao milele?

    Ni kipindi kirefu sasa kumekuwepo aina hii ya utapeli tulioubatiza jina la “TUMA KWA NAMBA HII”. Wapo waliofanikiwa kukwepa na wapo waliolizwa, na bado kuna wahanga watarajiwa. Haya yanatokea hata baada ya zoezi la usajili wa laini za simu ambao uliaminisha wengi ungekuwa suluhu ya jambo hili...
Back
Top Bottom