Katika kuendeleza dhamira yake ya kuthamini na kuhimiza uzalishaji wa maudhui yenye ubora na tija mtandaoni, JamiiForums usiku wa leo, wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Shindano la Stories of Change 2024, inawatambua Wanachama wake watano waliotoa michango chanya mwaka huu 2024...