Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna viongozi wa mikoa na wilaya wanaendeleza matumizi mabaya ya madaraka hasa eneo la ukamataji.
Rais Samia amesema hayo wakati akitoa hotuba baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Haki Jinai iliyotolewa na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo...