Heshima sana wanajamvi,
Kila mwanajamvi alijua msimamo wangu sina haja ya kuendeleza ligi uchaguzi umekwisha Lissu na Heche ni washindi.
Nawapongeza Lissu na Team yake ya kampeni kwa kazi kubwa sana.
Nilitaka uongozi wa Mbowe uendele lakini wenye chama waliona ni vyema wakabadilisha uongozi...
Mgombea wa Uenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, amewasili Mlimani City akiwa ndani ya gari alilopigiwa risasi na watu wasiojulikana mjiji Dodoma mwaka 2017 likiwa bado na alama za risasi katika ubavu wa kushoto ambao alikaa wakati akishambuliwa, ambapo leo Januari 21, 2025 unafanyika uchaguzi...
Moses Mgao, Mwenyekiti CHADEMA Jimbo la Kibaha Mjini amesema haya akiongea na waandishi wa habari
"Napenda kutangaza rasmi, sisi wanachama wa CHADEMA kutoka Mkoa wa Pwani na hasa watu wa Kibaha tumeamu tunakwenda kumpigia kura Mhe. Tundu Lissu awe Mwenyekiti wetu"