Ni kawaida sana kuona watu wakifuga kuku, ng'ombe, mbuzi, nguruwe, n.k. Lakini ni nadra sana kuona watu wakifuga samaki licha ya kuwa mazingira yetu yanafaa sana kwa shughuli za ufugaji samaki kutokana na kuwepo kwa maeneo yenye maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa. Baadhi ya mataifa kama China...