Wadau wa MMU tuongee Mahusiano Ijumaa ya leo
Kuna baadhi ya Wapenzi wakikosana hupigana kama njia ya kuonesha hasira zao
Lakini leo tuko na Wanaume. Kwa Mwanaume kumpiga mpenzi wake inaonesha nani ni 'kiongozi' ndani
Au wengine huamini Mwanamke bila kumpiga hasikii na habadiliki
Lakini...
Kwenye ulimwengu wa mahusiano kuna mtindo saivi kwamba wa kwanza kumpotezea, kumchunia au kumuacha mwenzake ndo mshindi, sio mtindo mzuri ni utoto.
Kama kweli mnajaliana mtaongea na kusuluhisha tatizo lililopo ila ikitokea mwanamke amekupotezea ujue upendo wake umepungua, mwache aende zake...