Wakati suala la ajira, kuboresha elimu, matumizi ya teknolojia vikitawala, vijana wametaka dira ya Taifa 2050 ipunguze umri wa watu kustaafu kwa lazima hadi kufikia miaka 55 kutoka 60.
Hayo yamesemwa leo Desemba 18, 2024 wakati vijana wakitoa maoni yao kwenye rasimu ya Dira ya Taifa 2050...