Habari,
Nimeenda NSSF kufuatilia mafao ya mirathi ya marehemu mzazi wangu aliyefariki akiwa kazini bado lakini cha kushangaza NSSF wanasema hatuna haki ya kupata mirathi hiyo kwasababu watoto wake tumezidi miaka 18 na hizo pesa ni mali ya serikali na NSSF.
Naomba kujua hii sheria imeanza lini...
Mimi ni mtoto wa marehemu ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF amefariki akiwa na umri wa miaka 57 lakini alikuwa bado hajastaafu.
Marehemu hakuwa na mume, na wazazi wake wote wawili walishafariki na sisi tupo wawili, lakini wote tuna miaka zaidi ya 25.
Nimeenda kudai mafao NSSF Ilala...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.