Ripoti mpya ya UN Women inaonyesha kuwa wanawake na wasichana 85,000 waliuawa kimakusudi na wanaume mwaka 2023, ambapo asilimia 60 (51,100) ya vifo hivyo vilitokea mikononi mwa wenza au wanafamilia wa karibu. Hii inathibitisha kuwa nyumbani, mahali ambapo wanawake wanapaswa kuwa salama zaidi...