Matamshi ya chuki, propaganda za kisiasa na uongo si matatizo mapya mtandaoni, nyakati za uchaguzi kama hizi huzidisha zaidi matatizo hayo. Matumizi ya roboti, au akaunti bandia (Feki) za mitandao ya kijamii, imerahisisha zaidi kueneza habari zisizo sahihi kimakusudi, pamoja na uvumi usio sahihi...