Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ameutaka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) pamoja na vyombo vingine vya usafiri ndani ya maji kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali ya usalama kwenye vivuko kwa kuhakikisha hawazidishi abiria wala mizigo ili kulinda usalama wa abiria pamoja na mali zao...