Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Uvuvi wa Comoro, Mhe. Dkt. Stanley Ali Bandar. Mazungumzo yao yalijikita katika namna Tanzania na Comoro zinavyoweza kuboresha ushirikiano katika sekta hizo mbili za Uvuvi na Kilimo...