USIMDHARAU MTU
1.
Za kale hapo zamani, hadithi inaanzia,
Yamhusu Yasmini, binti aliyevutia,
Mnene wa wastani, watu aliwazuzua,
Usimdharau mtu, ungali humfahamu.
2.
Juma mwana mtulivu, wa familya masikini,
Alikuwa si muovu, mwerevu pia makini,
Hakuwa mwenye uchovu, kumwendea Yasmini...