Niko zangu kibandani kwangu, hua nauza nguo kwa jumla na rejareja. Mara ghafula wanatokea watu wawili wachafu, mzee kwa umri zaidi ya miaka sitini akiwa amevalia suruali yenye viraka kila sehemu ila sehemu inayoonekana zaidi ni maeneo ya kwenye zipu ambapo pameshonwa na uzi mweupe wakati suruali...