Mnamo tarehe 06.03.2022 majira ya saa 18:00 jioni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Mtaa wa Mwanyanje – Uyole, Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya na kufanikiwa kumkamata ABDUL MWAKALINGA [27] Dereva Tax, Mkazi wa Uyole akiwa na bidhaa zilizozuiliwa kuingizwa nchini...