Tokea mwaka 1944, baada ya kutengeneza mfumo wa Bretton-Woods hakuna taifa ambalo limewahi kuwa na uchumi mkubwa kama Marekani. Kufika mwaka 1945, Marekani ilikuwa inamiliki nusu nzima ya uchumi wa dunia. Fedha ya Marekani ikishikiliwa na dhahabu (Gold-Backed) ilikuwa ndiyo inatumiwa kwa kiwango...