Kwa kuangalia upande wa madhaifu ya timu zote mbili katika mizani, naona Vipers wakiwa na safu butu mno ya ushambuliaji. Wamecheza michezo zaidi ya mitano pasipo kupachika goli hata moja, hivyo sioni namna wanayoweza kupata point tatu leo dhidi ya Simba. Mechi itaisha kwa Simba kushinda ama sare.