Hivi karibuni katika eneo la Buguruni kumekuwa na unyang'anyi ambao hufanywa kwenye mida ya saa 10 mpaka saa 11 alfajiri. Wezi hao wamegawanyika katika makundi mawili; kuna ambao hutembea kwa vikundi na hubeba silaha kama visu na ambao hutumia bodaboda. Wanawavizia watu ambao wanaenda kazini...