Ukweli sio kama ni mbaya au mchungu kama wasemavyo wahenga, ila uchungu na ubaya wake huja kulingana na maandalizi ya kuupokea. Ukitayarisha akili yako kupokea ukweli wakati wowote wala haitokuwia ugumu kuukubali na kuendelea na maisha yako. Tatizo ni pale tu ukweli unapokuja kisha hukuandaa...