Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Albogast Kajungu, amefanya ziara ya kushtukiza katika mashamba ya wakulima mbalimbali eneo la Mang’ola wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha na kuridhishwa na namna wakulima hao wanavyozingatia matumizi ya vipimo sahihi...