Na James Mbotela.
MUHTASARI WA MAISHA YA MWANDISHI
Mwandishi wa kitabu hiki, ni mzaliwa wa Frere Town, Kisauni, Mombasa. Baba yake ni Myao, akiitwa Mbotela ambaye alikuwa mmoja wa vijana wale waliookolewa baharini na Wazungu wa manowari za Waingereza zilizokuwa zikizuia biashara ya watumwa...