Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Innocent Chengula (23) kwenda jela miaka saba, baada ya kupatikana na makosa sita likiwamo la kujipatia Sh4 milioni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete...