02/02/2020 ni mwisho au mwanzo mpya wa Nabii na mtume Mwamposa?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hii tarehe ya leo tarakimu zake zimekaa vizuri sana ni 0 na 2 basi.

Leo ndio siku ambayo Nabii na mtume Mwamposya amekamatwa na jeshi la polisi na kwa maana hiyo atalala rumande nadhani ni mara ya kwanza tokea apate daraja la Utume.

Siku hii haitasahaulika kwa waumini wake iwe positively au negatively.

Nawatakia dominica ya 02/02/2020 yenye baraka!
 
Haya mambo bwana, ni mazito!! Labda serikali imuchukulie hatua kali za kisheria, ndio unaweza kuwa mwisho wake, lakini kwa akili za kiafrika, usije shangaa ndio ukawa ufunuo wake!!! Waumini wake wakawa. Mala kumi ya sasa!!
 
Hata hivyo kapiga mabilioni mengi sana tena bila kulipa kodi zetu. Huyu anatakiwa kupigwa money laundering akapumzishwe "store".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri serikali ipige marufufuku kabisa hii biashara ya uuzaji wa mafuta ya upako na maji ya upako.
Wafuasi wake nashangaa bado wameshupaza shingo kumtetea kana kwamba anafata maagizo ya Mungu.
 
Kwani Mwamposa kaua mtu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…