10,000$ kwenda kununua bidhaa China

Jan-uary

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
984
Reaction score
1,058
Nina hicho kiasi cha pesa,nataka nikanunue simu China niuze mkoani,je itanilipa?nipeni uzoefu wenu.
 
Ukitaka kufanya biashara yoyote lazima ufanye kwanza market research, ujue kama huko unakotaka kwenda kuuza hizo bidhaa kuna uhitaji kweli? Kama ukijiridhisha pia utaangalia bidhaa unayotaka kupeleka humu ina bei inayoendana na maisha ya wakazi wa huko?


Kama jibu ni ndio basi utarudi kwenye upande wa pili, utaangalia masoko ambapo unaweza kupata hizo bidhaa. Je soko gani unaweza kuzipata hizo bidhaa kwa bei nzuri na bila longolongo? Unakuwa na options nyingi, yawezekana ukawaza China kumbe labda Dubai ungeweza kupata mzigo kwa bei nzuri zaidi na kupunguza gharama (ni mfano tu)

So kabla hujaamua kuwekeza hiyo million 20+ jaribu kufanya mambo hayo muhimu
 
Nina hicho kiasi cha pesa,nataka nikanunue simu China niuze mkoani,je itanilipa?nipeni uzoefu wenu.

Mm nimefanya iyo biashara ya simu sana so nakupa ushaur tu , ni biashara ina challenge sana lazima upate mtu atakayekusasaidi coz simu za china refublish
So sina sumbua sana mkuu,kama unataka kuuza mkoa ni mkoa gani coz mikoan ni kazi sana kupata mtu anaweza nunua iphone so lazima ujue wanaweza kununua izo simu unazotaka kuuza
Biashara ya simu ndugu ni kazi sana lazima ununue sehemu wanayoweza kubadilisha izo simu kama zinasumbua so lazima ununue kwa mchina anayejua soko la tanzania
Kuna simu unaweza nunua china ukaleta hapa bongo unashangaa hawezi kufanya ussd code yan hawwzi fanya mpesa au tigo pesa ile menu
Na nunua simu za bei ya chini coz ndio rahisi kuuza na siyo simu za milion faida yake ni ndogo sana na ngunu kuuza
 
Mkuu , fanya utafiti wa soko la vifungashio vya bidhaa, wajasiliamali wengi wanalalamika sana kuwa ni adimu na wengine huagiza kenya, Nasikia china vinapatikana kwa wingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…