10 worst things in Nature

10 worst things in Nature

vivaforever

Senior Member
Joined
May 30, 2016
Posts
113
Reaction score
165
10Honey Badger
Mnyama mgomvi.
maxresdefault.jpg


Huyu jamaa kashindikana, yaani ni Kichwa cha Mwendawazimu kabisaa. Honey badger kama Waswahili tumwitavyo “Nyegere mara nyingi hupatikana Afrika na Kusini Magharibi ya Asia.

Kwa muda wa Miaka mingi sasa kitabu cha Rekodi za Dunia {Guinness Book of Records} kinamtaja Nyegere kuwa ndiye Mnyama asiye na hofu hata kidogo. Huyu mnyama (kwa kumwangalia tuu macho yako yanakudanganya unahisi ni mzuri) atashambulia chochote kile kinachokatiza mbele yake na pia ni mjanja sana anazijua sehemu dhaifu zote za adui yake. Mfano; akikutana na Binadamu mwanaume basi anamshambulia Pumbu zake.

Pia ni moja kati ya Wanyama wachache sana wanaotumia Vifaa, mfano; anatumia Magogo kama ngazi. Huyu mnyama anapenda asali balaa yaani anaweza kuingia kwenye mzinga wa nyuki bila kujali usalama wake kitu ambacho mara nyingi kinasababisha kifo chake. Huyu jamaa anaweza kuua Mamba pia ni muuaji mzuri wa Nyoka, anatumia dakika kumi na tano tuu kumla nyoka mwenye futi kumi na Tano. Uhuni wa huyu mnyama unajulikana kiasi kwamba hata Chui na Simba wanamkimbia .

9.Mbu
Mdudu mbaya zaidi.
mosquito-NationalGeographic_2197799.ngsversion.1516899610652.adapt.1900.1.jpg


Hakuna shaka kwamba mbu ndiye mdudu mbaya zaidi ulimwenguni. Msimu wa Joto ukianza tuu basi hawa jamaa hao huibuka na kuanza kushambulia miguu ya Binadamu kujipatia mlo. Usiku ukiwa umelala utawasikia wanang’ong’a lakini hata huwaoni yaani Usumbufu tuu.

Oh – pia ndiye mdudu anayeonekana hatari sana kwa kusambaza magonjwa kama vile Malaria, Matende na mabusha, Homa ya Manjano, Homa ya Dengue nk, Inaaminika kwamba nusu ya idadi ya watu ulimwenguni imekufa kutokana na kung’atwa na Mbu jike aina ya Anopheles. Utani kidogo; “Mungu huenda alikuwa kajisahau kipindi anaumba Wanyama maana nahisi Shetani alikuwa busy anajiumbia Mbu kule.”


8.Fatal Familial Insomnia
Gonjwa lenye Dalili mbaya sana

insonia-familiar-fatal_29766_l.jpg


Fatal Familial Insomnia, kwa kawaida Insomnia ni hali ya kukosa usingizi ila kwa kutafsiri ugonjwa huu ni kwamba “Ugonjwa wa kukosa wa usingizi wa Kifamila unaoleta Kifo”, ni Ugonjwa mbaya sana ambao unapatikana katika Familia 28 tuu ulimwengumi kote.

Huu Ugonjwa humzuia mtu asipate Usingizi na hakuna dawa hata moja inayoweza kumsaidia apate usingizi. Ugonjwa ukishakuanza, basi utaanza kukosa Usingizi usiku kwa muda wa miezi 7 hadi 38 hadi mwishowe unafariki. Dalili zake hujumuisha Kukosa usingizi mfululizo, Kusahau [Dementia], Kuona Maluweluwe [Hallucinations], Kupoteza uzito kupindukia na Paranoia.

7.Bullet Ant
King’ato kinachouma hatari

bullet-ant-glove-pain.jpg


The bullet ant (Siafu risasi) huyu ndiye anasemakana kuwa mwenye maumivu makali zaidi akikung’ata – mara nyingi analinganishwaga na maimivu ya kupigwa Risasi, akielezewa kama hivi: “mawimbi ya kuchoma, kugandamiza, aina zote za maumivu huku yakiendelea kuwepo kwa Masaa 24 mfululizo”.

Huyu siafu hupatikana Nicaragua kusini kwa Paraguay na, kama siafu wengine tuu, huishi kwa makundi makubwa chini ya Miti. Wakiamua kukushambulia wanakuja kundi zima, kama wewe umechill sebuleni kwako na kitambi chako pale basi utahama bila kubeba vitu vyako.

Katika kabila la Satere-Mawe huko Brazil, hawa siafu hutumika kama Sehemu ya kuanzishia shughuri zao za kimila kwa vijana. Vijana huvalishwa Gloves zikiwa na Mamilion ya siafu wanaachwa wang’atwe kwa kama dakika 10 hivi na lazima warudie baada ya siku kadhaa. Mikono yao mara nyingi huwa ina[paralyse huku miili yao ikitetemeka kwa siku kadhaa.

6.Salvinia Molesta
Mmea vamizi zaidi.

Pia hujulikana kama Magugu ya Kariba (kariba weed), huu mmea ni umeshindikana kwa kweli. Salvinia molesta ni mmea jamii ya fern plants {wale wa O level kwenye Bilology tulisomaga kuhusu Fern plants}.

Huu mmea huelea juu ya Maji na kuongezeka ukubwa mara mbili yake kila baada ya siku chache. Huu mmea ndio unaosababisha baadhi ya maziwa kufunikwa kabisa kiasi kwamba hata maji yasionekane. Huu mmea huzuia Mwanga wa jua usiingie ndani ya Maji mwishowe kufanya Vimbe vya majini visiweze kuishi. Kuifanya hali iwe mbaya zaidi,huwezi kuua huu mmea, ukiukata vipande vipande basi kila kipande kitakua Mmea mpya tena unakua haraka sana kipindi cha uchanga wake. Huu mmea sasa unapatikana karibia kila mahali Duniani huku ukisababisha matatizo kila sehemu unapochipukia. Katika hiyo picha unayoiona unaweza kudhani ni Uwanja mzuri uliofunikwa na nyasi, usijihadae, hilo ni Ziwa limefunikwa na salvinia molesta.

5. Corpse Flower
Ua linalonuka vibaya zaidi, yaani kama Maiti vile

corpse-flower-titan-arum-eden-project-open-802234.jpg

The corpse flower hustawi katika ardhi ya Majani inayopakana na Misitu ya Mvua huko Sumatra (Ingawa kwa sasa unapatikana maeneo mbalimbali Duniani katika bustani za maonyesho).

Huu mmea hutoa ua moja tuu ambalo hukua pia hutoa harufu mbaya sana inayofanana kwa alimia kubwa na Maiti inayooza (ndipo linapotoka jina lake). Hili ua hukua kwa zaidi ya futi 10 kiupana na rangi yake inaiga rangi ya Maiti inayooza. Kikonyo cha Ua hili kina joto sawa na mwili wa binadamu jambo ambalo huenda likawa linachangia harufu mbaya na kuleta illusion kwamba kuna maiti inayooza kweli.

4
.Brazilian Wandering Spider
Buibui mbaya zaidi

Phoneutria-bahiensis.jpg


Ni mkubwa. Ana maumivu makali zaidi akikung’ata kuliko wote kwatika ulimwengu wa Buibui. Ni buibui mbaya sana (Badass); sahau buibui aina ya funnel web spider – hiki kitu ni Hatari kwa kweli. Huyu ndiye Buibui aliyeua idadi kubwa ya watu Duniani. Na kuifanya hali iwe mbaya sana, huyu Buibui akikung’ata anasababisha mwanaume apate Erection (Uume kusimama) kwa masaa kadhaa. Onyo –msije mkadhani hii ni Viagra; Sumu ya huyu Buibui kwa sasa wanasayansi wanaisoma ili kujua kama inaweza kutumiwa kutibu Tatizo la mwanaume kutokusimamisha (ERECTILE DYSFUCTION)

3.Candiru
Samaki Mkorofi sana

CANDIRU-dest.jpg


Candiru ni samaki mdogo sana ambaye anapatikana katika mto Amazon huko Amerika ya Kusini ambapo yeye ndiye samaki anayeogopwa zaidi tena kuliko samaki aina ya Paranha.Huyu samaki anaweza kukua kufikia Inchi Sita. Candiru anajipatia Chakula kwa kunyonya damu za Viumbe wengine ambapo huogelea kwa kutumia Mapezi (Gills) kufuata mawindo yake na hutumia Miba kali kama nyembe zilizopo kichwani mwake kujishikiza katika mwili wa Windo lake. Hutafuna ngozi ya windo lake hadi kuffikia mshipa mkubwa wowote ule wa damu ambapo hunyonya Damu hadi aridhike.

PHuyu samaki huyapata mawindo yake kwa kunusa maji, wana uwezo mkubwa wa kuvuta harufu ya mkojo wa Binadamu ambapo hufuata huo mkojo hadi kwenye sehemu za siri za mttu harafu huigilia kupitia hapo. Akiingia husababisha maumivu makali sana kwa Binadamu na hawezi kutoka isipokuwa kupitia Upasuaji tuu.

2. Binadamu
Kiumbe Muharibifu zaidi katika Mazingira

full_35271.jpg

Kabla sijaanza kujisimanga na kukusimanga wewe hebu tuweke mambo sawa kwanza – Mimi sio Mtunza mazingira wala Mpenda mazingira mzuri – lakini hata mtu mwenye moyo mgumu asiyeweza kurecycle takataka kama mimi anaweza kuona Uharibifu tunaoufanya katika MazingiraTun achafua njia za maji, hewa, tunakata misitu yote, tunaharibu majabali, na tunafukia taka za Nyuklia chini ya Ardhi.

Mazingira ya Asili (Nature) yana kila sababu ya kutuchikia huenda hiyo ndo ikawa sababu ya sisi kupigwa na majanga kama vile Vimbunga, Tauni, Magonjwa ya mlipuko nk.

1.Botulinum Toxin
Sumu mbaya sana

botulinum-toxin-500x500.jpg


Botulinum toxin (Sumu ya Botulinum) huzalishwa na Bakteria anayejulikana kama Clostridium botulinum na bila shaka ndiyo Protini hatari zaidi inayojulikana Duniani.

Kama Clostridium botulinum ataingiza Spore zake katika Chakula au Kidonda, ataanza kutoa sumu ambazo zinaharibu Tishu za Mwili au kukifanya chakula kiwe sumu kikiliwa. Hii sumu ni Hatari sana kiasi kwamba Paundi mbili tuu (1kg) inatosha kuua idadi yote ya watu ulimwenguni. Kutokana na kuwa na sumu kali sana, Nchi nyingi ulimwenguni hutumia hii sumu kama silaha ya Maangamizi ya Kibaiolojia (Biological Weapon of Mass destruction).

Kitu cha aina hii wote tunaweza sema tukae mbali nacho, au sio? Si hivyo, hapana. Mamilion ya Watu wanajichoma hii Protini katika nyuso zao kila Mwaka; Hii Protini hupatikana kwa kiwango kidogo sana katika Botox ambayo ni dawa inayotumika kutibu makunyanzi usoni.

KARIBUNI. 🙂🙂🙂
 
Mkuu hiyo namba 1 maelezo yake sio kweli, Botulinum Toxin sio Nature product hiyo ni Lab product. Tena zipo type A, B, C, D, E, F, G na H. Hatari unayoiongelea ni hiyo type H. Hiyo picha inaonyesha type A ambayo ya kawaida haiui ila inasababisha ugonjwa tu.
Matumizi ya kawaida tu ya botox ni pamoja na kubana uke, kurudisha misuli iliyolegea, kuondoa uzee etc.
At least ungeweka majanga ya asili kama Ukame, Mafuriko, Radi, Matetemeko hapo sawa!.
Botox type H zinatengenezwa jeshini sio kitu cha asili mkuu!.
 
Haha kuna haja ya kuzuia uzalishaji wa hiyo sumu ya Clostridium botulinum. Na wale wanaozuia uzee kwa kuapply usoni vipodozi mbalimbali vya Botix kuondoa mikunjo wajue kabisa wanapunguza umri wao wa kuishi kwa kasi sana.
 
Mkuu hiyo namba 1 maelezo yake sio kweli, Botulinum Toxin sio Nature product hiyo ni Lab product. Tena zipo type A, B, C, D, E, F, G na H. Hatari unayoiongelea ni hiyo type H. Hiyo picha inaonyesha type A ambayo ya kawaida haiui ila inasababisha ugonjwa tu.
Matumizi ya kawaida tu ya botox ni pamoja na kubana uke, kurudisha misuli iliyolegea, kuondoa uzee etc.
At least ungeweka majanga ya asili kama Ukame, Mafuriko, Radi, Matetemeko hapo sawa!.
Botox type H zinatengenezwa jeshini sio kitu cha asili mkuu!.[/QUOT

Sikuwa na mda wa kudadavua sana maana kutype thread ndefu kupitia Smartphone ni shidaa, pia hiyo picha nimeiweka tuu maana ningeweke ya mechanisms yake ingekuwa inaleta confusion kwa wengine. Kuhusu kutengenezwa ukae ukijua hata zile Gangrenes kama Gas gangrene ni outcomes za C.botulinum toxins ila haimaanishi hao Bacteria wametoka Lab ndo wakaenda kuvamia kidonda bali ni Naturally occuring in Nature
 
Haha kuna haja ya kuzuia uzalishaji wa hiyo sumu ya Clostridium botulinum. Na wale wanaozuia uzee kwa kuapply usoni vipodozi mbalimbali vya Botix kuondoa mikunjo wajue kabisa wanapunguza umri wao wa kuishi kwa kasi sana.

Kweli kabisa kaka ila sema ndo hivyo wakina dada zetu hasa ndo wameangukia kwenye huo mtego
 
Kweli kabisa kaka ila sema ndo hivyo wakina dada zetu hasa ndo wameangukia kwenye huo mtego
Wazungu wana njia nyingi sana za kuua taratibu vizazi vya kiafrika na kupunguza uwezo wa waafrika wa kufikiri ili wao waendelee kudominate utawala wao juu yetu. Aina mbali mbali za sumu zinazoua na kusababisha magonjwa mbali mbali zimewekwa kwenye vyakura, maji hadi kwenye madawa ya binadamu tunayotumia. They are called sedatives
 
Back
Top Bottom