Zakumi,
Hata kama kusingekuwepo na external factors, mipango yote ya 1971-1981 were doomed to fail kwa sababu moja kubwa tu waTanzania hawakuwa source ya maendeleo yao.
Huwezi kutumia pesa na kuomba omba na kukopa kujenga maendeleo bila ya wewe mwenyewe kuwa na shughuli za ku-sustain maendeleo hayo.
Mkuu wangu hatubishani isipokuwa tunaelimishana kwa faida ya wote wanaosoma hapa..
Sijasema una spin, isipokuwa unapotosha kwa sababu unashindwa kuweka taarifa zako wazi..na hakuna sehemu nimezungumzia external wala internal factors.. hizi zipo kila nchi duniani iwe kwa maendeleo yao ama kuanguka kwao.. mimi sipo huko!
Nachozungumza mimi ni hali ya uchumi Tanzania nyakati mbili na vipimo ulivyotumia sijasema sababu kwani binafsi naamini kabisa kwamba bila mikopo ama omba omba tusingekuwa na muindombinu iliyojengwa..Na mara zote ktk uchumi unapojenga miundombinu ni kutokana na malengo ya kuongeza uzalishaji baadaye sio wakati unapojenga iwe ndio kipimo cha mauzo..Ila una create ajira, misingi na vyanzo vya uzalishaji.
Hata wewe mkuu wangu unapojenga nyumba (iwe guest house) pato au akiba yako haiwezi kuwa sawa na siku utakapo anza kupangisha nyumba hiyo..Ujenzi unaweza kukusukuma kuchukua mikopo na kuonekana omba omba lakini kwa mwenye kujua maana na soko la guesthouse atasema Zakumi ana akili kweli..
Tatizo langu ni ktk kutazama matumizi ya mikopo tuliyochukua. Nyerere alichukua mikopo na akaifanyia kazi kujenga misingi na vyazo vya uzalishaji tofauti na mikopo inayochukuliwa leo kukidhi mahitaji yasiyokuwa ya lazima na ndio maana tuna matatizo ya Umeme, maji, Afya, Elimu, Usafiri, na Uzalishaji wenyewe kwa sababu tumeshindwa kuweka misingi bora kulingana na ongezeko la watu na mahitaji yetu...
Nakuomba usome tena ile hotuba ya Mwalimu ambayo aliitoa baada ya Azimio la Arusha, nini malengo na misingi ya kukopa fedha kwani kukopa sio haramu ktk maendeleo ya Kiuchumi iwe kwa nchi ama mtu binafsi..
Bill Gates alikopa akawa omba omba na kila mwaka mikopo ilizidi ukubwa kulingana na mahitaji ya shirika lake hadi siku alipoanza kuzalisha na kupeleka mali yake sokoni ndipo tumeona maendeleo yake..
Binafsi naamini kabisa kwamba tuli fail kwa sababu ya mwongozo - SIASA ilokuwa ikituendesha pamoja na matatizo mengine ya nje.. ni somo kwetu lakini hatuwezi kujenga kambi ktk sababu zile kupindisha ukweli kwamba leo hii tunavuruga.. Obama amekabidhiwa nchi ina madeni ni jukumu lake kusoma alama na makosa yaliyopita kisiasa na Kiuchumi kuweza kusonga mbele lakini ni ujinga kutumia kipimo cha failure za Bush kujaribu kujenga hoja kwa nini atashindwa kufanikiwa..
Kiongozi bora ni yulke anayetazama beyond failure zilizopita na kuahidi wananchi kuwatoa ktk matatizo hayo na hata kuboresha nguzo za uchumi kwa kuweka misingi bora zaidi siyo kutumia matatizo yaliyopita kuonyesha udhaifu unaotokea ktk Utawala wake..