15 November ...snowhite alizaliwa!

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,065
Reaction score
24,559
rafiki na wapendwa wangu!leo ni siku yangu ya kuzaliwa

Namshukuru sana MUUMBA kwa baraka na baraka tele alizonijalia na pumzi anazonijaalia toka nilipozaliwa mpaka sasa

HAKIKA SIFA NA UTUKUFU NI WAKE

Namshukuru sana mama yangu kwa kunizaa na kunilea toka nikiwa tumboni mpaka aliponiacha na kurudi kwa Muumba wake,natamani sana angepata heri ya kuniona nikiwa sasa mama, mke najua na naamini angejivunia sana mimi

HAKIKA NAKUPENDA NA KUKUMBUKA SANA MAMA YANGU

Namshukuru sana baba yangu kwa kunileta duniani na kunilea, yeye amekuwa nguzo yangu na amani yangu mpaka aliponiacha naye kumrudi kwa Muumba wake, naye natamani sana angenishuhudia leo nikiwa ni mwanamke jasiri na shupavu kama alivopenda niwe

HAKIKA I MISS YU daddy,(mwenyewe alikuwa ananiita mama yangu coz nilipewa jina la bibi yangu)

Namshukuru sana mume wangu, amekuwa ni rafiki mpenzi kwa maisha yangu miaka 17 pamoja naye haikuwahi kuwa majuto kwenye maisha yangu!

HAKIKA NAKUPENDA UPEO MAISHA YANGU!(mie humwita NAFSI YANGU MIMI)

Nawashukuru sana watoto wangu, wamekuwa furaha na faraja ya pekee sana kwa maisha yangu wamekuwa zaidi ya watoto wangu, infanct ni mashosti zangu, nawapenda sana na hawajanidissappoint as a mother! I'm very proud of them

HAKIKA NAMASHUKURU MUNGU KWA AJILI YAO

Nawashukuru sana dada zangu,kaka zangu
najua nilivyokuwa mtundu na wa kudeka enzi hizo

MUNGU AWABARIKI SANA KWA KUNIFUNDISHA YOTE!tatizo tu hesabu ndo zilikataa kupanda!

JF friends!
You guys sijui niseme nini kuonyesha kuwa nawapenda sana kila mmoja kwa nafasi na upekee wake FP we unajua ni dada mkubwa, thank you very much for being one gfsonwin weye mwali hata sina maneno ya kukwambia, thank yu very much The Boss we ni big brother si unajua? Ahsante sana kwa kuwa hivyo Ciello wewe ni mamduchu enh? Yap i love you dogo BAK hujawahi kunidisappoint kwenye upande wa miburudiko ahsante brother Boflo ah we mtu sijui nisemeje, jua tu unanipa cheko na bashasha kwa post zako, af nakumbushia ile offer yangu ya massage treat! cacico mke mwenza we wajua vile u remind of those days! SnowBall mtoto wa kiume wa mama yangu thank yu pacha watu8 ahahahahhahhaha ahsante sana kwa mambo yetu yaleeee! Hujawahi kuniangusha si unajua? Kaizer na Asprin mimi proud being ur mwalimu bana lara 1 kino gal, hujawahi kunibore kwa uandishi wako, I like ur style girl!
MJ'r partner shukrani sana kwa kushare nami interest kwenye ushairi Kongosho bi harusi wangu, mimi love you kwa kweli, na ahid ya glambox lazima niitimize Zinduna Madame B , mwaJ na King'asti ndani ya chama letu kubwa nawapenda sana mashosti Mtambuzi mume ya mama ngina wewe lol!ahahahhahhhha love yu sana bana Dark City,HORSE POWER na Mkusa hongera sana kwa mawazo yenu

Well idadi ni kubwa saaaan nashindwa kuimaliza. Wengine woote NAWAPENDA SANA SANA SANA SANA!
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana kwa siku yako hii njema. Mwenyezi Mungu azidi kukubariki na aibariki familia yako. Akuongezee maisha marefu yenye amani na furaha. Siku zako zikapate kuwa nyingi zenye mapenzi mema kutoka kwa wale wote wakupendao. Heri ya siku yako ya kuzaliwa.
 
Happy Birthday Dada Snowhite! Nina zawadi ya Likungu kutoka ziwa nyasa, upo wapi nikuletee??

Allah akujalie afya njema, maisha ya furaha na huyo shemeji yetu, maisha marefu na Mwenyezi Mungu akutimizie kila hitaji la Moyo wako!!!
 
Happy Birthday Mwalimu wangu.

Hongera kwa kufikisha miaka 30!

Mungu yu mwema kwako, mshukuru na mtumikie.

na we nawe nilijua tu utasema lione!
aahahhahahha haya bana!hapo tu unajifanya kudai shikamoo kijanja!
luv yu sana Asprin
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…