1786 kulikua na shreia na taratibu za kufuata ukichukua chumba Guest House

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1635964501667.png
 
Imeielewa vipi! ! hii english ya shakespear!! please ebu niume sikio!

zamani shule nilikuwa drama club. play za 'hamlet', 'romeo and juliet' 'othello' nilizisoma soma kidogo nakupata japo kitu.

ingawa hicho kipande nilichotafsiri nimefanya hivyo kuweka ka context ya kibongo bonge. najua 'wench' maanake ni mhudumu au mfanyakazi wa kike kwa english ya zamani, ingawa ilitumika zaidi pia kumaanisha makahaba. nikajiongeza tu kwenye kutafsiri kwa sababu ya kuleta ujumbe kwetu wazee wa kushika shika mabaamedi
 
Daaa! sawa kaka mkubwa!! mliosoma enzi za mkoloni mlifaidi sana!!...... kimbembe ni hizi shule za kata Maweeee!! sijui zamani za ''UPE ndo kabisaaa!!! yaani Elimu ya Bongo bana!! siki hizi ukienda hapo tu south unapigwa msasa upya!

Ila Elimu ya south ukienda UK! ni ajira moja kwa moja!
 
😀 sijasoma enzi za mkoloni mkuu. labda sikutakiwa kutumia neno 'zamani'. nna miaka 36 tu 😀😀 huenda hata wewe umenizidi umri 😀😀
 
Yaani mkuu! sheeda sana hizi shule zetu wewe!! umesoma Tanganyika IST ile ya masaki nini? manake sisi bana ni huko mbwinde huko karibu na Lukunyu! au kikomera!! kule bana gari halifiki!!

yaani unatembeaaaaaa!! unafika mahali unapanda kimtumbwi cha kuendesha mwenyewe! ukifika ng'ambo ya pili unakiacha hapo! unatembea tena mbele ivovivo! mpaka unavuka vivuko km 4 ivi! ndo unafika kijijini kwetu kuzuri sana hallow!

Hiyo habari mie naona ni kizungu mkuti tu! kwanza nashukuru kukaa mjini Bongo!! kamwe sikutamani tena kurudi kule hallow! ebu fikiria mjini nyama kila siku! tena fresh! chai kila siku,tena na vitafunwa! kule sukari mbinde!!

zahanati ya kijiji bado ina sindano za kuchemsha! tena wana noa kwenye jiwe lilee la kunolea panga! lkn nilipokuja huku mjini lool! raha ilioje sindano zinatupwa! kamwe sintarudi asante shule!
 
Naluelewa mkuu. Nilisoma shule nzuri sana kwa kweli, nadhani inaendana na IST 😀😀. Darasani tukiwa 30 tunaonekana wengi sana. Aina ya shule nnayotamani wanangu wasome pia. Wanafunzi wanachochewa kuwa wabunifu. Walimu wanafundisha kwa nia na kujadiliana na wanafunzi, siyo kufoka foka na fimbo. Ubunifu unapewa kipaumbele na kila somo linaumuhimu sawa na lingine siyo yale mambo ya 'sciences ni bora kuliko arts' na kila mwanafunzi anaaminishwa atatoboa katika sekta yoyote apendayo. Library ina vitabu kama vyote so nilikuwa nashinda huko nasoma kila topic niipendayo kuanzia wanyama na samaki, hollywood film industry hadi shakespeare (hii yote ni kujisomea mwenyewe siyo kusukumwa usome).

Pia ulikuwa na kipindi kinaitwa 'library' kama nakumbuka vizuri. Darasa zima linaenda library na kazi ya mwanafunzi hapo ni kuchagua kitabu chochote na kujisosomea kwa dk. 30 - 60. Ukikutwa huna kitabu unakula adhabu. Wa kusoma 'sungura na fisi', haya. Wa kusoma 'quantum physics' haya...mwisho wa siku mwanafunzi anajikuta anajua mengi na naamini inaboresha maisha yake ndani na nje ya nafsi yake. Inamsaidia mwanafunzi kutambua ni nini anapenda na inamsaidia kuamua mapema anataka kufuata taaluma gani baadae. Na wanajifunza kufikiria 'nje ya box'.

Suala la shule za vijijini na hali zake linanisikitisha mpaka leo na katika michango yangu midogo ya kijamii, nachangia kwenye elimu.
 
Back
Top Bottom