Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Kipindi cha 18 Matatizo ya Kiafya ya Kawaida wakati wa Ujauzito
Utangulizi
Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu matatizo matatu ya kawaida ya kiafya wakati wa ujauzito na athari zake kwa afya ya mjamzito: malaria, anemia na maambukizi kwenye njia ya mkojo na jinsi ya kutofautisha maambukizi ya njia ya mkojo (MNM) yanayoweza kutibiwa kutokana na yale yanayoendelea kwa kibofu cha mkojo na ugonjwa kali unoathiri figo. Tutakueleza visababishi, ishara, dalili, utambuzi, na udhibiti wa hali hizi, na wakati wa kumpa mama rufaa kwa kituo cha afya kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Na utajifunza njia bora za kuzuia hali hizi zisitokee na umuhimu wa kufanya hivyo hasa wakati wa ujauzito.
Malengo ya Somo la Kipindi cha 18
Ukimaliza kipindi hiki, unapaswa kuwa na uwezo wa:
18.1 Kufafanua na kutumia kwa ufasaha maneno yote muhimu yaliyochapishwa kwa herufi nzito. (Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 18.1 na 18.2)
18.2 Kueleza hatari kwa mama, fetasi na mtoto mchanga za malaria, anemia na maambukizi kwenye njia ya mkojo wakati wa ujauzito. (Swali la Kujitathmini 18.1)
18.3 Kuwashauri wajawazito na waume zao jinsi ya kuzuia malaria, anemia, na maambukizi kwenye njia ya mkojo. (Swali la Kujitathmini 18.2)
18.4 Kutambua ishara na dalili za malaria kwa mjamzito, na kujua jinsi ya kudhibiti na wakati wa kumpa mama rufaa kwa kituo cha afya. (Swali la Kujitathmini 18.2)
18.5 Kutambua dalili za anemia kwa mjamzito, na kujua jinsi ya kudhibiti na wakati wa kumpa mama rufaa kwenye kituo cha afya. (Swali la Kujitathmini 18.2)
18.6 Kubainisha na kutofautisha kati ya ishara na dalili za maambukizi kwenye njia ya mkojo na ya figo wakati wa ujauzito, kudhibiti maambukizi yasiyokali kwenye njia ya mkojo wakati wa ujauzito na dawa za kumeza na kutambua wakati wa kumpa mama aliye na maambukizi yanayoendelea rufaa kwenye kituo cha afya. (Swali la Kujitathmini 18.2)
Mchoro 18.1 Baadhi ya aina ya mbu wanaoweza kusambaza parasiti za malaria kwa watu.
18.1 Malaria wakati wa ujauzito
Malaria ni maambukizi ya seli nyekundu za damu inayosababishwa na parasiti iitwayo Plasmodiumu zinazobebwa na aina fulani ya mbu. Mbu hutoa parasiti za malaria katika damu ya mtu aliyeambukizwa anaponyonya damu 'chakula', na kisha kupitisha parasiti anapomwuma mtu mwingine (Mchoro 18.1). Parasiti hukua na kukomaa katika seli nyekundu za damu na mamilioni ya parasiti hukusanyika katika plasenta ya mjamzito.
Malaria inaweza kuwa kali zaidi kwa kina mama walio na magonjwa mengine. Malaria ni hatari zaidi kwa wajawazito kuliko watu wengine. Mjamzito aliye na malaria yuko katika hali ya kupata anemia (utakavyoona baadaye katika kipindi hiki), kuharibika kwa mimba (kutoka kwa mimba pekee yake kabla ya wiki 24 za ujauzito), kuzaa mapema, kupata mtoto mdogo zaidi, kuzaa mtoto aliyekufa (mtoto kuzaliwa akiwa amekufa baada ya wiki 24 za ujauzito) au kufa yeye mwenyewe (kifo cha mama).
18.1.1 Dalili za malaria
Dalili za ugonjwa huwa ishara kwa mwathiriwa na anazifahamu na kuwa na uwezo wa kukueleza kuzihusu; wanaweza kukuambia pekee yao, lakini unaweza kuuliza maswali yanayozihusu. Dalili za malaria ni kama vile:
Mchoro 18.2 Mtu aliye na joto jingi mwilini atahisi joto zaidi kukuliko.
Ishara za ugonjwa ni ishara kuwa mhudumu wa afya pekee ndiye atakaye jua, au kutambua kwa kufanya uchunguzi. Kwa mfano, ukishuku ni malaria, unapaswa kupima halijoto na kipimajoto ukiwa nacho (ulijifunza jinsi ya kutekeleza haya katika Kipindi cha 9 ), au kwa kulinganisha hali yako ya joto na ya mama (Mchoro 18.2). Mtu akiwa na malaria, joto mwili linaweza kwenda juu hadi sentigredi 39-40 au hata zaidi.
18.1.2 Utambuzi wa malaria
Kuna njia mbili kuu za kutambua malaria kwa kutumia uchunguzi wa damu. Njia rahisi ni kufanya uchunguzi wa haraka wa malaria ambao hutambua protini zinazotolewa na parasiti katika damu ya mgonjwa. Vifaa vya kuchunguza vinaweza kuwa aina ya vijiti vya kutumbukiza, plastiki, au kadi, ambazo hubadilisha rangi zinapopata tone la damu kutoka kwa mtu aliyeambukizwa - kwa kawaida huchukuliwa kutoka kwa kidole na shindano safi. Hata hivyo, vifaa vya kuchunguzia lazima vihifadhiwe kwa makini na kutunzwa kutokana na unyevu na joto jingi. Mafunzo kwa wahudumu wa afya yanahitajika kabla ya utambuzi sahihi wa ishara za malaria kwa malengo ya uchunguzi.
Njia nyingine ya kutambua malaria, ambayo inahitaji utaalamu wa mafunzo na vifaa, ni kutokana na uchunguzi wa damu kwa hadubini kwenye kioo, ambacho kimewekwa rangi ilikuonyesha parasiti. Vifaa vya kuchunguzia damu kwa hadubini kwa kawaida havipatikani katika Kituo cha Afya cha ngazi ya chini. Ikiwa umefunzwa kufanya uchunguzi wa malaria wa haraka na unaweza kutumia vifaa vya kufanyia uchunguzi, unapaswa kutoa utambuzi wa malaria kutokana na malengo ya uchunguzi huu. Ikiwa huwezi kutumia vifaa vya kuchunguza malaria kwa haraka, tekeleza utambuzi wako kwa msingi wa dalili (kwa mfano, maumivu ya kichwa, joto jingi mwilini, baridi, maumivu katika misuli /viungo), na joto jingi mwilini iliyopimwa na kipimajoto.
18.1.3 Matibabu ya malaria wakati wa ujauzito
Ni muhimu kwa wajawazito kuepukana na malaria - au kutibiwa haraka wakiwa wagonjwa. Dawa za kutibu malaria zinaweza kuwa na madhara, lakini ni afadhali kuliko kupatwa na malaria. Ikiwa mama ana dalili za malaria, anapaswa kutibiwa mara moja. Dawa inayotumika mara nyingi huitwa Artemether Lumifantrine(Inauzwa kama Coartem). Uharibu ukuaji wa parasiti katika seli nyekundu za damu za mtu.
Coartem inaweza kutumika kutibu malaria katika awamu ya pili na ya tatu ya ujauzito. Awamu ya pili ni wiki 13-27 tangu wakati wa mwisho wa mama kupata hedhi ya kawaida, na awamu ya tatu ni kutoka wiki 28 hadi wakati wa kuzaa, karibu wiki 40. Malengo ya uchunguzi yakionyesha kuwepo kwa malaria, au ukishuku kuwepo kwa malaria sana kulingana na ishara na dalili, na mama akiwa katika awamu ya pili ama ya tatu, mtibu kama ilivyoainishwa katika Kisanduku 18.1.
Kisanduku 18.1 Kutibu kwa kutumia Coartem katika awamu ya pili au ya tatu ya ujauzito
Wajawazito wanaoshukiwa kuwa na malaria katika awamu ya kwanza ya ujauzito, wanaoweza kusafiri, wanapaswa kupelekwa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu kwa matibabu maalum.
Mama akiwa katika awamu ya kwanza ya ujauzito (yaani, hadi wiki 12 tangu wakati wa Mwisho wa mama Kupata Hedhi yake ya Kawaida), lakini anaugua sana kusafiri hadi kituo cha afya, mpe matibabu yaliyo katika Kisanduku 18.2. Hatari kwa maisha yake na ya fetasi kutokana na malaria, ni kubwa kuliko hatari ya kutumia dawa mapema wakati wa ujauzito. Mtume kwenye kituo cha afya haraka punde tu hali yake inapomruhusu kusafiri. Kumbuka kwamba dawa aina yaArtesunate huwekwa kwa kapsuli yenye umbo maalum - iitwayo sapozitori - katika njia ya haja kubwa kwa kusukuma polepole kupitia ------ wake.
Picha 18.3 Mhudumu wa Afya anaonyesha chati chenye tembe za Coartem katika makundi manne. (Picha: hisani ya AMREF)
Kisanduku 18.2 Sidano ya Artemether na ya Artesunate kupitishwa kwenye ------
Sindano ya Artemether hudungwa kwa misuli kabla ya rufaa hali kali za malaria inaposhukiwa. Kwa kipimo cha miligramu 3.2 ya Artemether kwa kila kilo ya uzani wa mama, katika dozi moja kwenye misuli ya mkono wake upande wa juu.
Artesunate hupitishwa kwenye ------ katika sapozitori kwa dozi zifuatazo kabla ya kupewa rufaa.
Kumbuka kwamba wajawazito wanaweza kuwa na uzani wa zaidi ya kilo 40 baada ya awamu ya kwanza ya ujauzito.
Jumla ya vifo vinavyotokana na malaria na magonjwa ya malaria zimepungua katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na jitihada kubwa za kuzuia malaria na matibabu ya haraka inapotokea. Mpango huu ni muhimu sana kwa kupunguza malaria hata zaidi, ikiwa ni pamoja na utambuzi na matibabu ya mapema kwa wajawazito wanaokuja kwenu kwa huduma ya ujauzito.
18.1.4 Kukinga malaria
Ili kukinga malaria, lazima ufanye lote uwezalo ili usiumwe na mbu. Unapaswa kushauri kila mtu katika jamii wajitokeze pamoja ili:
Picha 18.4 Vyandarua vilivyotiwa dawa ya kuua wadudu hutoa kinga nzuri kutokana na mbu wanaosambaza malaria. (Picha: UNICEF / Indrias Getachew)
Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii. Panga kufanya kampeni ya afya kwa lengo la kuhamasisha wana nchi namna ya kukinga malaria, kwa kutumia mbinu za kukuza afya ulizojifunza katika Kipindi cha 2 katika Moduli hii. Hakikisha kwamba wajawazito unao wahudumia wanajua kwamba, watoto wao ambao hawajazaliwa na walio chini ya miaka 5 wote wako katika hatari ya malaria.
18.2 Anemia katika ujauzito
Kina mama walio na anemia huwa na nguvu kidogo ya kuzaa na kuna uwezekano wa kuvuja damu sana baadaye (kuvunja damu nyingi baada ya kuzaa), wawe wagonjwa, au hata kufa baada ya kuzaa. Tayari umejifunza mengi kuhusu utambuzi na uzuiaji wa anemia katika vipindi vya mafunzo ya hapo awali katika Moduli hii, hivyo katika kipindi hiki tutazingatia tiba yake na kuimarisha ulichojifunza.
Kumbuka kwamba baadhi ya aina ya anemia husababishwa na ugonjwa sio ukosefu wa ayoni na baadhi hurithiwa kutoka kwa wazazi (maumbile). Inaweza pia kusababishwa na parasiti fulani, ikiwa ni pamoja na malaria na minyoo. Katika kipindi hiki, tunashughulikia anemia inayosababishwa na upungufu wa ayoni kwa chakula. Wajawazito wengi wana anemia, hasa wanawake walio maskini ambao hawawezi kula vyakula vyenye ayoni ya kutosha, kama unavyojua kutoka Kipindi cha 14.
18.2.1 Utambuzi wa anemia
Chunguza anemia kwa wajawazito wote kila mara wanapotembelea kliniki, kwa kuuliza kuhusu dalili zake. Maswali muhimu ya kuuliza ni:
Ishara za anemia (kinachochunguzwa au kupimwa na mhudumu wa afya) ni:
Ukishuku kuwa mama ana anemia, mshawishi afanyiwe uchunguzi wa anemia ikiwa huduma hiyo inapatikana katika Kituo cha Afya kilicho karibu. Uchunguzi wa damu hupima kiasi cha hemoglobini (ayoni iliyoko katika damu) ili kutathmini ikiwa inatosha kubeba oksijeni inayohitajika kwa shughuli za kawaida na mahitaji ya mtoto ambaye hajazaliwa kwa ukuaji. Ikiwa uchunguzi wa damu haupatikani, tumia utathimni wako wa ishara na dalili maalumu (zilizotajwa hapo juu) kutambua anemia na kutoa matibabu kama ilivyoelezwa hapo chini.
Kwa ziara ya baadaye wakati wa utunzaji katika ujauzito
Ukiwa na wasiwasi kuwa mjamzito ana anemia na haonyeshi maendeleo yoyote, unapaswa kumpa rufaa kwenye Kituo cha Afya mara moja.
18.2.2 Ukingaji wa anemia katika ujauzito
Kula lishe bora
Wajawazito wote lazima washauriwe wale vyakula vilivyo na viwango vya kutosha vya ayoni na folate (vitamini, ambayo pia huitwa folic acid). Tayari unafahamu ni kwa nini anahitaji ayoni. Folate pia husaidia kukinga anemia kwa wajawazito au wanaonyonyesha, na inaweza kukinga baadhi ya hitilafu za kimaumbile kwa mtoto.

- Baridi (kuhisi baridi isiyo ya kawaida) na kutetemeka (vipindi vikali vya kutetemeka kwa dakika kadhaa na hudumu hadi saa 1), hii huwa dalili ya kwanza ya maambukizi
- Maumivu ya kichwa na udhaifu mara nyingi huandamana na baridi
- Joto jingi mwilini (halijoto ya juu); Joto jingi mwilini mara nyingi hufuatwa na baridi, na joto linaweza kwenda juu sana hivyo mtu anakabiliwa na deliriumu(kutokuwa katika hali sawa kiakili, kuona au kusikia mambo yasiyohalisi)
- Kutokwa na jasho joto lishukapo
- Katika baadhi ya hali zingine kuhara/kutapika kunaweza pia kushuhudiwa
- Dalili nyingine ya kawaida ni maumivu ya misuli/viungo.
Mchoro 18.2 Mtu aliye na joto jingi mwilini atahisi joto zaidi kukuliko.
Ishara za ugonjwa ni ishara kuwa mhudumu wa afya pekee ndiye atakaye jua, au kutambua kwa kufanya uchunguzi. Kwa mfano, ukishuku ni malaria, unapaswa kupima halijoto na kipimajoto ukiwa nacho (ulijifunza jinsi ya kutekeleza haya katika Kipindi cha 9 ), au kwa kulinganisha hali yako ya joto na ya mama (Mchoro 18.2). Mtu akiwa na malaria, joto mwili linaweza kwenda juu hadi sentigredi 39-40 au hata zaidi.
- Ni ipi kiwango cha joto la mwili la kawaida na ishara ya joto jingi mwilini ni ipi?
- Joto la mwili kwa kawaida ni sentigredi 37; ishara ya joto mwilini litakuwa sentigredi 38 au zaidi.
Mwisho wa jibu
18.1.2 Utambuzi wa malaria
Kuna njia mbili kuu za kutambua malaria kwa kutumia uchunguzi wa damu. Njia rahisi ni kufanya uchunguzi wa haraka wa malaria ambao hutambua protini zinazotolewa na parasiti katika damu ya mgonjwa. Vifaa vya kuchunguza vinaweza kuwa aina ya vijiti vya kutumbukiza, plastiki, au kadi, ambazo hubadilisha rangi zinapopata tone la damu kutoka kwa mtu aliyeambukizwa - kwa kawaida huchukuliwa kutoka kwa kidole na shindano safi. Hata hivyo, vifaa vya kuchunguzia lazima vihifadhiwe kwa makini na kutunzwa kutokana na unyevu na joto jingi. Mafunzo kwa wahudumu wa afya yanahitajika kabla ya utambuzi sahihi wa ishara za malaria kwa malengo ya uchunguzi.
Njia nyingine ya kutambua malaria, ambayo inahitaji utaalamu wa mafunzo na vifaa, ni kutokana na uchunguzi wa damu kwa hadubini kwenye kioo, ambacho kimewekwa rangi ilikuonyesha parasiti. Vifaa vya kuchunguzia damu kwa hadubini kwa kawaida havipatikani katika Kituo cha Afya cha ngazi ya chini. Ikiwa umefunzwa kufanya uchunguzi wa malaria wa haraka na unaweza kutumia vifaa vya kufanyia uchunguzi, unapaswa kutoa utambuzi wa malaria kutokana na malengo ya uchunguzi huu. Ikiwa huwezi kutumia vifaa vya kuchunguza malaria kwa haraka, tekeleza utambuzi wako kwa msingi wa dalili (kwa mfano, maumivu ya kichwa, joto jingi mwilini, baridi, maumivu katika misuli /viungo), na joto jingi mwilini iliyopimwa na kipimajoto.
18.1.3 Matibabu ya malaria wakati wa ujauzito
Ni muhimu kwa wajawazito kuepukana na malaria - au kutibiwa haraka wakiwa wagonjwa. Dawa za kutibu malaria zinaweza kuwa na madhara, lakini ni afadhali kuliko kupatwa na malaria. Ikiwa mama ana dalili za malaria, anapaswa kutibiwa mara moja. Dawa inayotumika mara nyingi huitwa Artemether Lumifantrine(Inauzwa kama Coartem). Uharibu ukuaji wa parasiti katika seli nyekundu za damu za mtu.
Coartem inaweza kutumika kutibu malaria katika awamu ya pili na ya tatu ya ujauzito. Awamu ya pili ni wiki 13-27 tangu wakati wa mwisho wa mama kupata hedhi ya kawaida, na awamu ya tatu ni kutoka wiki 28 hadi wakati wa kuzaa, karibu wiki 40. Malengo ya uchunguzi yakionyesha kuwepo kwa malaria, au ukishuku kuwepo kwa malaria sana kulingana na ishara na dalili, na mama akiwa katika awamu ya pili ama ya tatu, mtibu kama ilivyoainishwa katika Kisanduku 18.1.
Kisanduku 18.1 Kutibu kwa kutumia Coartem katika awamu ya pili au ya tatu ya ujauzito
- Tembe 4 za Coartem mara mbili kwa siku (baada ya masaa 12) kwa siku 3 (jumla ya tembe 24). Mshauri ameze na chakula, maziwa, supu au uji wa shayiri. Anaweza kuzivunja na kuzichanganya kwa kijiko cha chakula kama hii itakuwa rahisi kwake kumeza dawa. Mchoro 18.3 inaonyesha jinsi ya kueleza kina mama idadi ya tembe za kumeza.
- Unaweza pia kumpatia tembe za paracetamol (miligramu 500-1000) kila baada ya saa 4-6 ili kupunguza joto jingi mwilini.
- Kupanguza mwili wake kwa kitambaa kilichoingizwa ndani ya maji baridi pia husaidia akiwa na joto jingi.
- Mshauri mama anywe maji mengi ili awe na maji ya kutosha mwilini. Anapaswa kunywa angalau kikombe1kubwa cha maji kila saa.
Mama akiwa katika awamu ya kwanza ya ujauzito (yaani, hadi wiki 12 tangu wakati wa Mwisho wa mama Kupata Hedhi yake ya Kawaida), lakini anaugua sana kusafiri hadi kituo cha afya, mpe matibabu yaliyo katika Kisanduku 18.2. Hatari kwa maisha yake na ya fetasi kutokana na malaria, ni kubwa kuliko hatari ya kutumia dawa mapema wakati wa ujauzito. Mtume kwenye kituo cha afya haraka punde tu hali yake inapomruhusu kusafiri. Kumbuka kwamba dawa aina yaArtesunate huwekwa kwa kapsuli yenye umbo maalum - iitwayo sapozitori - katika njia ya haja kubwa kwa kusukuma polepole kupitia ------ wake.
Picha 18.3 Mhudumu wa Afya anaonyesha chati chenye tembe za Coartem katika makundi manne. (Picha: hisani ya AMREF)
Kisanduku 18.2 Sidano ya Artemether na ya Artesunate kupitishwa kwenye ------
Sindano ya Artemether hudungwa kwa misuli kabla ya rufaa hali kali za malaria inaposhukiwa. Kwa kipimo cha miligramu 3.2 ya Artemether kwa kila kilo ya uzani wa mama, katika dozi moja kwenye misuli ya mkono wake upande wa juu.
Artesunate hupitishwa kwenye ------ katika sapozitori kwa dozi zifuatazo kabla ya kupewa rufaa.
| Uzani wa mama | Dozi | Idadi ya sapozitori |
|---|---|---|
| Kilo 30-39 | Miligramu 50 | 1 |
| Zaidi ya kilo 40 | Milingramu 400 | 4 |
Kumbuka kwamba wajawazito wanaweza kuwa na uzani wa zaidi ya kilo 40 baada ya awamu ya kwanza ya ujauzito.
Jumla ya vifo vinavyotokana na malaria na magonjwa ya malaria zimepungua katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na jitihada kubwa za kuzuia malaria na matibabu ya haraka inapotokea. Mpango huu ni muhimu sana kwa kupunguza malaria hata zaidi, ikiwa ni pamoja na utambuzi na matibabu ya mapema kwa wajawazito wanaokuja kwenu kwa huduma ya ujauzito.
18.1.4 Kukinga malaria
Ili kukinga malaria, lazima ufanye lote uwezalo ili usiumwe na mbu. Unapaswa kushauri kila mtu katika jamii wajitokeze pamoja ili:
- Kuondoa maji taka yanayoleta mbu; ondoa maji ya mvua kwenye choo; funika au ondoa makopo ya bati na sufuria zinazokusanya maji karibu na nyumba.
- Usikae usiku katika maeneo yenye maji ambapo mbu huzalia.
- Tumia vyandarua vilivyotiwa dawa ya kuua wadudu, kemikali inayoua mbu. Katika maeneo mengi, unaweza kusambaza vyandarua vilivyotiwa dawa ya kua wadudu (tazama Picha 18.4) kwa familia zinazozihitaji. Vyandarua hivi vinalinda watu ambao hulala ndani yao kutokana na mbu, na wao pia hupunguza hatari kwa wale wengine wanaolala katika chumba kimoja nao kwa sababu dawa hii hufukuza mbu wasiingie ndani ya nyumba.
Picha 18.4 Vyandarua vilivyotiwa dawa ya kuua wadudu hutoa kinga nzuri kutokana na mbu wanaosambaza malaria. (Picha: UNICEF / Indrias Getachew)
Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii. Panga kufanya kampeni ya afya kwa lengo la kuhamasisha wana nchi namna ya kukinga malaria, kwa kutumia mbinu za kukuza afya ulizojifunza katika Kipindi cha 2 katika Moduli hii. Hakikisha kwamba wajawazito unao wahudumia wanajua kwamba, watoto wao ambao hawajazaliwa na walio chini ya miaka 5 wote wako katika hatari ya malaria.
18.2 Anemia katika ujauzito
Kina mama walio na anemia huwa na nguvu kidogo ya kuzaa na kuna uwezekano wa kuvuja damu sana baadaye (kuvunja damu nyingi baada ya kuzaa), wawe wagonjwa, au hata kufa baada ya kuzaa. Tayari umejifunza mengi kuhusu utambuzi na uzuiaji wa anemia katika vipindi vya mafunzo ya hapo awali katika Moduli hii, hivyo katika kipindi hiki tutazingatia tiba yake na kuimarisha ulichojifunza.
- Je, anemia ni nini na nini hutokea katika mwili wa mtu aliye na anemia?
- Mtu akiwa na anemia, kwa kawaida inamaanisha kuwa hajala vyakula vyenye ayoni ya kutosha. Seli nyekundu za damu huhitaji ayoni kutengenezahemoglobini, kiungo kinachosaidia seli nyekundu za damu kubeba oksijeni kutoka kwa hewa tunayopumua hadi sehemu zote za mwili. Mtu aliye na anemia hawezi kutengeneza seli nyekundu za damu za kutosha, hivyo mwili wao una upungufu wa oksijeni.
Mwisho wa jibu
Kumbuka kwamba baadhi ya aina ya anemia husababishwa na ugonjwa sio ukosefu wa ayoni na baadhi hurithiwa kutoka kwa wazazi (maumbile). Inaweza pia kusababishwa na parasiti fulani, ikiwa ni pamoja na malaria na minyoo. Katika kipindi hiki, tunashughulikia anemia inayosababishwa na upungufu wa ayoni kwa chakula. Wajawazito wengi wana anemia, hasa wanawake walio maskini ambao hawawezi kula vyakula vyenye ayoni ya kutosha, kama unavyojua kutoka Kipindi cha 14.
18.2.1 Utambuzi wa anemia
Chunguza anemia kwa wajawazito wote kila mara wanapotembelea kliniki, kwa kuuliza kuhusu dalili zake. Maswali muhimu ya kuuliza ni:
- 'Je, unajihisi mdhaifu au kuwa mchovu kwa urahisi?'
- 'Je, unashindwa kupumua (upungufu wa pumzi) unapofanya kazi za kinyumbani?'
- 'Je, unapata kizunguzungu mara nyingi, na umewahi kuzirai (kukosa fahamu)?
Ishara za anemia (kinachochunguzwa au kupimwa na mhudumu wa afya) ni:
- Weupe: uweupe ndani ya kope la jicho, viganja vya mikono, kucha, na ufizi.
- Kupumua kwa kasi (zaidi ya mara 40 kwa dakika; kawaida kiwango cha kupumua ni mara18-30 kwa dakika).
- Mpigo wa haraka kwa mshipa (zaidi ya mipigo100 kwa dakika). Ulijifunza jinsi ya kupima kiwango cha mipigo kwa mshipa katika Kipindi cha 9 (Sehemu ya 9.4).
Ukishuku kuwa mama ana anemia, mshawishi afanyiwe uchunguzi wa anemia ikiwa huduma hiyo inapatikana katika Kituo cha Afya kilicho karibu. Uchunguzi wa damu hupima kiasi cha hemoglobini (ayoni iliyoko katika damu) ili kutathmini ikiwa inatosha kubeba oksijeni inayohitajika kwa shughuli za kawaida na mahitaji ya mtoto ambaye hajazaliwa kwa ukuaji. Ikiwa uchunguzi wa damu haupatikani, tumia utathimni wako wa ishara na dalili maalumu (zilizotajwa hapo juu) kutambua anemia na kutoa matibabu kama ilivyoelezwa hapo chini.
Kwa ziara ya baadaye wakati wa utunzaji katika ujauzito
- Chunguza weupe ndani ya kope la macho yake, mikononi, kucha, na ufizi.
- Hesabu mipigo wa mshipa wake. Je, ni zaidi ya 100 kwa dakika?
- Hesabu mipigo anazopumua katika dakika 1. Je, ni zaidi ya 40?
18.2.2 Ukingaji wa anemia katika ujauzito
Kula lishe bora
Wajawazito wote lazima washauriwe wale vyakula vilivyo na viwango vya kutosha vya ayoni na folate (vitamini, ambayo pia huitwa folic acid). Tayari unafahamu ni kwa nini anahitaji ayoni. Folate pia husaidia kukinga anemia kwa wajawazito au wanaonyonyesha, na inaweza kukinga baadhi ya hitilafu za kimaumbile kwa mtoto.
- Rejelea Kipindi cha 13. Taja baadhi ya vyakula ambavyo vina ayoni nyingi.
- Unaweza kuwa umefikiria baadhi ya vyakula hivi: kuku, samaki, alizeti, malenge na boga mbegu; maharagwe, mbaazi na dengu; mboga zenye rangi ya kijani kibichi; viazi vikuu; boga ngumu; nyama nyekundu (hasa ini, figo na nyama zingine za ogani); bidhaa za nafaka nzima kama vile mkate wa hudhurungi; mikate iliyowekwa ayoni (iliyoongezwa); karanga na kiini cha yai.
Mwisho wa jibu
- Taja baadhi ya vyakula vilivyo na folate nyingi.
- Samaki; alizeti, malenge, na boga, mbegu; maharagwe na mbaazi; mboga zenye rangi ya kijani kibichi; nyama nyekundu (hasa ini, figo, na nyama nyingine); mchele wa hudhurungi; ngano nzima; uyoga na mayai.