1960s: Kisa cha Balozi Malaya wa Ufaransa na Majasusi wa Kike wa Russia (Femme Fatales)

Hii stori nzuri sana. Ukiipost kwa kiingereza itanoga zaidi, Kiswahili chake hapa kinakuwa kigumu kidogo kueleweka vizuri
 
mkuu, ina maana wewe ni mtu wa Nigeria na haujui Kiswahili vizuri?
Kiswahili ni lugha yangu ya pili. Kwa hiyo ni kati ya lugha ambayo ninaijua katika nafasi ya pili, wakati Kiingereza nakijua katika nafasi ya tatu. Kama umewahi kusoma sana makala pamoja na novels, mara nyingi zinapotafsiriwa kutoka Kiingereza kuja Kiswahili, zinakuwa ngumu zaidi kueleweka kwa lugha ya Kiswahili kuliko ile ya awali ambayo ni Kiingereza. Kwa mfano halisi, kuna Riwaya moja ya Chinua Achebe inaitwa "No longer at Ease". Hii riwaya niliwahi kuipata ikiwa imetafsiriwa kwa Kiswahili nikajaribu kuisoma, wala sikuambulia kitu, huwezi kuielewa lakini kwa Kiingereza inaelewewka. Hapa inabidi tukubaliane kitu kimoja kuwa kuna baadhi ya makala zikitafsiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, zinakuwa ngumu zaidi kuzielewa kwa Kiswahili kuliko kwa Kiingereza.
By the way, naturally Kiswahili ni kigumu kuliko Kiingereza, sema tu kwa sababu sisi Kiingereza siyo lugha yetu ya kwanza!
 
Unataka na Kihehe pia? Kihehe na Kisukuma vinashahibiana, tutakuwa tunaweka Kisukuma ili na wajukuu zetu mao wawe wanaelewa. Karibu usukuma Christmas mjukuu ukanywe maziwa ya ng'ombe
sawa babu nitakuja huko Usukumani ila ninaogopa sana Gambosh kutokana na story ninazozisikia
 
Duuuuh hao KGB wanaonekana walikuwa ni moto wa kuotea mbali. Kumbe mpaka wanawake wanaweza kuwa majasusi hatari namna hiyo?
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Mkuu, mbona hata Kagame anatumia wanawake, kwani hujui kuwa wanawake warembo wa Kinyaruanda wamejaaa Tanzania kwa kazi za ujasusi!!
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Mkuu, mbona hata Kagame anatumia wanawake, kwani hujui kuwa wanawake warembo wa Kinyaruanda wamejaaa Tanzania kwa kazi za ujasusi!!
Mkuu, sijawahi kulifahamu hili hapo kabla. Sasa mbona inakuwa ni rahisi kutambulika kama wapo too obvious namna hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…