Ukweli sijajua kipi ni kipi ,,, lakin navyoona mimi nikama jeshi letu yani TPDF linasifika sana ndani ya mipaka ya Tanzania ( kwa watz ) ,,, lakini nje ya mipaka ya Tz habari ni tofauti inaonekana ni jeshi la kawaida tu
Ukiangalia kinachoendelea sasa hivi Congo ,, utaona wa -congo wengi wakishukuru jeshi la south Africa na malawi tu ,,, sasa huwa najiuliza mbona hawaishukuru na Tz ?? Basi naishia kukaa kimya huenda jeshi letu linapiga kazi kimya kimya
Lakin pia ,, ukija upande wa nguvu ,, utaona jeshi la Kenya (KDF )kwa upande wa East Africa linaonekana ndiyo jeshi lenye nguvu zaidi hii imechochewa zaidi na kikosi maalumu cha jeshi la kenya kwenda kwenye operation maalumu ya kusimamia Amani huko haiti nadhani misheni hii imelipa jeshi la kenya extra credit na kufanya nchi kubwa kama marekani kuona kuwa linawez kufanya kitu katika huu mgogoro unaondelea pale Congo unlike their neighbors Tanzania and Uganda who have never done any recognized and successful mission outside their Continent .. hivyo hatuna budi kukubali kuwa Kenya ni giant in East Africa almost in Everything