Kuna wauliza maswali ambao majibu yao yameshajibiwa hapo juu katika sehemu napoainisha sababu moja inayopelekea kila mmojawapo kuwa miongini mwa vijana 10 wenye mvuto/ushawishi zaidi nchini. Sasa ngoja nijaribu kujibu maswali mapya yaliyoibuka hapo juu:
Kuhusu huyo Mwanamasoko, naongelea zaidi ushawishi wake katika kuwafikia watu wengi zaidi na zao lao - ZAIN, hapo siongeli VODA au TIGO.
Kuhusiana na suala la umri nimeshakubali hoja, ndio maana kina Michuzi nimeshawatoa kwenye hiyo 10 bora, sina uhakika kuhusu Shigongo.
Kuwahusu hao Ze Komedi, hapo siwezi kupinga, vijana hao wanastahili sana hasa kwenye ushawishi wao wa kubadilia lugha tunayoitumia.