Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
mwaka 2005 uligombea ukiwa umehitimu kidato cha sita. Mwaka 2010 bado elimu yako ni hiyo hiyo ya kidato cha sita. Ubungo watakuuliza umeshindwa kumaliza shule yako mwenyewe utawezaje kuleta maendeleo?Mwenzio Nape alikwenda kusoma India baada tu ya uchaguzi. wewe na chadema tu
Hao walosoma wamefanya nini la maana kumzidi Mnyika?
Nchimbi PhD
Chenge LLB,LLM(Harvard)
Prof.Ndulu
Prof.Yule waubalozi Italia
The list goes on...come on its what is in your heart and head man
Safari,
Pamoja na madudu waliyofanya hao wasomi wetu lakini isiwe kigezo cha kudharau elimu.
Mimi bado naamini elimu ndio mkombozi wa Mtanzania mmoja mmoja na pia taifa.
Kama mtu anaona ana mapungufu sehemu ni bora akasoma na sasa tuna bahati ya kuwa na OUT.
Muhimu tu ni lengo la kusoma liwe kukusaidia kuziba mapengo yalipo katika utendaji wako na wala sio kuongeza idadi ya vyeti vya kutundika ukutani na kuweka kwenye CV hata kama havikuongezei tija au uwezo wa kufanya kazi zako. Vyeti kama hivyo ni udanganyifu kwako mwenyewe na nchi yako.
Ongelea masuala muhimu sana sio maisha ya watu kama hivi. Ndio sisi tunaanza kuleta haja ya mtazamo wa ajabu jaribu kujikita zaidi kwenye hoja za Mnyika na sio hivi ilivyoUko sahihi kabisa Ndugu Mwananchi.Mimi nimeongelea kwa context ya Mnyika kuishia Darasa la kumi na nne kamailivyodaiwa hapo awali ingawa sina hakika na hilo labda John afafanue ''Kijiswali hiki''
Hoja ya ukabila huwa inajitokeza, na kwa kweli ni hoja ya kukemewa. Ni ubaguzi ambao Mwalimu Nyerere aliwahi kuuita ni sawa na kula nyama ya mtu. Ndugu wa karibu wa ukabila ni udini, nao huwa unasema semwa. 2005 niligombea na Keenja, ni mchagga. Mimi ni chotara wa kiafrika- baba yangu msukuma wa mwanza, mama yangu ni mpare wa same. Kwa hiyo wakati huo nilipochukua fomu, wapo walioniasa kwamba usigombee kwa kuwa wewe sio mchagga, kwa hiyo wachagga wa ubungo hawatakuunga mkono. Kama ningesikiliza sauti hizo wakati huo, hata ule ushindani wa 2005 ambao mpaka leo umebaki kuwa sehemu muhimu ya historia usingekuwepo. Nikaingia, na kwa kweli ni nikaungwa mkono na watanzania, wa makabila mbalimbali wanaoishi ubungo; wakiwemo wachagga. Sasa tuendelee na mjadala wazi kwa kweli, hiyo ilikuwa 2005; je, 2010 hali imebadilika na kwamba sasa jimbo la Ubungo lina ukabila wa hali ya juu na kwamba makabila mengine yasigombee jimbo hilo ndani ya Mkoa wa Dar es salaam?
Pamoja ya kuwa ninakubaliana na kuwa kuna tabia ya BAADHI ya wapiga kura kupenda kuomba pesa kutoka kwa wagombea, vile vile naunga mkono hoja ya Mnyika kuwa sio wote wenye mtazamo wa kuchagua kwa kupewa pesa. Na actually wengi wao hawapendi tabia hiyo. Hawapendi pia kudanganywa, maana ni watu wenye heshima zao na vipesa vidogo vidogo wanaviona kama vinawavunjia heshima tu. Japokuwa kama wengine, hupenda kuonyeshwa kuwa mgombea anawajali pia.Kwa hiyo changamoto kuu niliokuwa nayo kama mgombea wakati huo ilikuwa si tu kuwaeleza sera zangu nakusudia kufanya nini bali pia kuwabadili mtizamo(mindset/perception) kwamba mgombea hapaswi kugawa fedha. Na kwa kweli mwanzoni ilikuwa ngumu sana, lakini niliamua kabisa kampeni zangu msingi wake mkuu uwe ni kufanya siasa safi na kutoa elimu ya uraia.
Unaweza kuona namna ambavyo vuguvugu hili likuja kukubali; na kwa kweli wakati huo tuliweza kushindana na chama dola, na mgombea aliyekuwa waziri wakati huo akichangiwa na wafanyabiashara wakubwa akigombea kwenye chama chenye tuhuma ya kuchota fedha kifisadi na kuchangiwa na mafisadi.
Hoja yangu kuu ndani ya makala yangu; je uamuzi wa kugombea au kutogombea kwa mgombea ambaye tayari anafahamika mbele ya umma nguvu na udhaifu wake; je uwe suala lake binafsi au uhusishe pia maoni ya umma?
Nimekusoma bwana mzee na pia sasa ni wakati mwafaka watu kama nyinyi wote mkaunga mkono watu makini na wagombea makini kama wakina Mnyika na kujitokeza kabisa ili kufanya Tanzania iwe imara kabisaJosh,
Labda umepandia njiani katika hoja hii.Mimi napingana na mchangiaji aliyepekenua elimu elimu ya Mnyika.I will keep mum anyway....