2010; World Cup ya kiwango cha chini katika historia ya miaka ya karibuni...

2010; World Cup ya kiwango cha chini katika historia ya miaka ya karibuni...

Ramos

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2010
Posts
498
Reaction score
130
Kwa wafuatiliaji wa WC ya mwaka huu watakubaliana na wachambuzi mbalimbali wa soka duniani kuwa haya ndiyo mashindano yaliyotia fora kwa kiwango duni kati ya mashindano matano (au zaidi), ya miaka ya karibuni. Ndiyo mashindano ambayo waamuzi ama kwa makusudi au kwa ufinyu wa ujuzi wameboronga zaiai, na ndiyo mashindano yaliyoongoza kwa kuwa na warusha maonyesho ya TV wenye viwango duni zaidi hata ikilinganishwa na ligi za mataifa kadhaa... It is so sad!!!!!!!!!!
 
Kweli kabisa. Officiating ya mwaka huu ni ya ajabu na mbaya sana. World Cup niliyoipenda mimi ni USA '94.
 
Kweli kabisa. Officiating ya mwaka huu ni ya ajabu na mbaya sana. World Cup niliyoipenda mimi ni USA '94.

Kabisa nami ndiyo maana nasema kama wanataka kuilinda reputation ya kandanda basi hawana jinsi bali kuruhusu instant replay kabla ya mwisho wa mwaka huu.
 
controversies zinaleta raha ya mchezo kumbuka!

Haya Mkuu...lakini kama sikosei wapenzi na mashabiki wa kandanda duniani wengi watapenda kuona Bingwa halali na siyo anayepatikana katika maamuzi yaliyojaa makosa chungu nzima toka kwa Waamuzi.
 
Haya Mkuu...lakini kama sikosei wapenzi na mashabiki wa kandanda duniani wengi watapenda kuona Bingwa halali na siyo anayepatikana katika maamuzi yaliyojaa makosa chungu nzima toka kwa Waamuzi.

Kiongozi kama umecheza mpira na refarii akatoa maamuzi ya kukupendelea nadhani huwa na furaha sana ila ni shubiri kwenye timu pinzani! all in all there is lots of unfairness!
 
afadhali mimi si mchezaji wa mpira kiasi cha kuingia mashindano makubwa, ningemfanyia fujo refa tu, huwezi kuvumilia ujinga kama huu.
 
Kiongozi kama umecheza mpira na refarii akatoa maamuzi ya kukuendelea nadhni huwa na furaha sana ila ni shubiri kwenye timu pinzani! all in all there is lots of unfairness!

Mpira nimeucheza sana Mkuu...In order to maintain the reputation of the beautiful game, FIFA should introduce instant replay asap so as to reduce human errors.
 
Nyie timu zenu mnazopendelea zimetolewa mnaleta longo longo sasa, Argentina oyeeeeeeeeeeeee!!!!!!
 
Ovyo kabisa refereeing! Nini point ya kuangalia mechi kama inakuwa decided na maamuzi ovyo ya refa? Bora warushe sarafu tu! Hata NBA ambapo watu wanafunga hundreds of points bado kuna instant replay, kwenye mpira ambapo goli moja lina uzito sana hakuna!

Pia waanze kuwapunish wachezaji post game for diving, yaani mechi nzima watu wanajirusha tu utazani wanapigwa risasi!
 
Wakuu napingana na nyie mlio wengi - kiwango cha Ujerumani, Mexico, Urugway, Ghana, Brazil, Spain na Agentina ni kizuri sana. Mfano game ya jana kati ya Argentina na Mexico ilikuwa ya kiwango cha juu mno ni kati ya game nzuri so far.

Tutaona viwango safi hasa kwa hizi timu za America ya kusini wanacheza mpira wa kasi sana. angalia magoli ya jana lile moja na mexico na lile la mbali la Tevez - angalia movements wanapokuwa na mpira utapenda.

Still to come jamani - timu zilozotoka ndiyo zilikuwa zinadororesha mashindano haya zimeshatoka - timu kama uingereza jamani? hata kama wangepewa goli la Lampard lakini sijaona kitu wamefanya, kweli soka ya uingereza ina tatizo kubwa, something has to be done faster. kuna mdau amesema anamkosa Gaucho - mi nafikiri gaucho alikuwepo kwenye timu ya Mexico yule kijana machachari sana jina limenitoka ila wadau mtamkumbuka tu ana kasi mjanja sana. tutamkosa sababu timu yake bora imetolewa na timu bora zaidi.
 
Kwa wafuatiliaji wa WC ya mwaka huu watakubaliana na wachambuzi mbalimbali wa soka duniani kuwa haya ndiyo mashindano yaliyotia fora kwa kiwango duni kati ya mashindano matano (au zaidi), ya miaka ya karibuni. Ndiyo mashindano ambayo waamuzi ama kwa makusudi au kwa ufinyu wa ujuzi wameboronga zaiai, na ndiyo mashindano yaliyoongoza kwa kuwa na warusha maonyesho ya TV wenye viwango duni zaidi hata ikilinganishwa na ligi za mataifa kadhaa... It is so sad!!!!!!!!!!

Mkuu naomba nikupinge sana tu!!!

hatuwezi ku-generalise kwamba kiwango cha weldi kapu kimeisha wakati ndio kwanza tuko half way!!! judgement ya kwamba ni mbaya inategemea factors nyingi sana, kuanzia maandalizi, ulinzi ubora wa mechi, vitendea kazi, timu zenyewe na hata broadcasting

so far ukiondoa controversies za refariis, mengine yako better sana [labda na mavuzizela ambayo siyapendi]. in fact hata group stages zimetoa very good indication kwamba its no longer a walk over weldi kapu kama miaka ya nyuma... tumeona new zealand, australia, sauzi afrika, slovakia, serbia, uswisi wakitoa kamasi magwiji... tumeona england, italy na france wakiangukia pua... tumekumbushwa na kameruni na naijeria kwamba jina is nothing in modern soccer...KWANGU MIMI NAAMINI HIZI NDIZO CHACHANDU ZA WELDI KAPU

Weldi kapu hii imenoga na inaonyesha sasa power ya modern soccer inavyoswihi, angalia tactics --- u miss your opponent plan umepigwa kitu

Naamini mleta mada umechagua baadhi ya vigezo na kuweka hapa... mimi nashauri tuendelee kuiangalia na mwisho ndio tuhukumu

btw, usitegemee western media wakaisifia saaana african weldi kapu, kumbuka waingereza walishaanza zamamni sana kuipiga vita nk.

hayo ya refa ni mapungufu na rest assured kila anayeboronga anastahili teh next plane out!!!
 
Kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya waamuzi ,matukio mengine ni unfair.Nakumbuka France walivyoqualify ,timu kubwa bado zinapewa upendeleo
 
Kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya waamuzi ,matukio mengine ni unfair.Nakumbuka France walivyoqualify ,timu kubwa bado zinapewa upendeleo

Mkuu Belo, wewe na wadau wengine tutasema hivyo sababu tu timu ya Uingeleza imekataliwa goli lao- lakini kumbuka tukianza kutumia video kuhakiki magoli mpira hautanoga tena. angalia goli la Teves lile ka kuotea, ni kweli aliotea lakini ile movement kabla ya yeye kumalizia lile goli ilikuwa classic kiasi cha kuwachangaya waamuzi - Tukichokonoa chokonoa sana tutaharibu uhondo wandugu.

Kwa wengi kutolewa kwa Uingeleza, Ufaransa na Italy ni misiba lakini bahati mbaya hizi timu hazikuwa na mpira wa kasi na dunia ya leo bila kasi na pasi za haraka haraka unapigwa tu.
 
Nyie timu zenu mnazopendelea zimetolewa mnaleta longo longo sasa, Argentina oyeeeeeeeeeeeee!!!!!!

Mkuu umesema ukweli - watu wamesusa mashindano haya kisa timu zao zimetolewa. Mkuu Argentina ni class ingine - unanikumbusha goli la 3 la Tevez dhidi ya Mexixo jana. Jamaa yupo juu.
 
Mkuu Belo, wewe na wadau wengine tutasema hivyo sababu tu timu ya Uingeleza imekataliwa goli lao- lakini kumbuka tukianza kutumia video kuhakiki magoli mpira hautanoga tena. angalia goli la Teves lile ka kuotea, ni kweli aliotea lakini ile movement kabla ya yeye kumalizia lile goli ilikuwa classic kiasi cha kuwachangaya waamuzi - Tukichokonoa chokonoa sana tutaharibu uhondo wandugu.

Kwa wengi kutolewa kwa Uingeleza, Ufaransa na Italy ni misiba lakini bahati mbaya hizi timu hazikuwa na mpira wa kasi na dunia ya leo bila kasi na pasi za haraka haraka unapigwa tu.

true mazee... we jiulize marekani in two games alinyimwa mabao mawili.... na media iliishia kusema they are unlucky!!! sasa la ingreza limekuja basi ni kasheshe
 
hii ni the best worldcup, wanaosema ni mbaya ni kwamba timu zao zimetolewa baaasi, mexico super, ghana wako juu ukiondoa matatizo ya umaliziaji, ureno kamwonyesha brazil kuwa ukikaa vibaya na kombe huchukui, argentina safi zaidi ya mexico, uingereza pumba za mwaka ndo maana wakachezea kichapo cha mbwa mwizi toka kwa wajeru,tatizo watu wanapenda kuendeshwa na historia, kwamba uingereza hajafungwa na ujerumani since 1966, mara oohh france ndo sijui nn, those things are outter control these days, matatizo yaliyopo ukiondoa maamuzi mabovu ambalo ni tatizo la fifa the rest ni matatizo ya kawaida ambayo hutokea kila mara kutegemea na mahali world cup ilipofanyika...SA wamejitahidi sana na naamini some of the wazungu walokuwa siku zote wanaona Afrika kwa ujumla wake ni nothing watakuwa mpaka sasa wanashangazwa na everything they see down in mzansi!!lets be realistic guys..
 
Mkuu Belo, wewe na wadau wengine tutasema hivyo sababu tu timu ya Uingeleza imekataliwa goli lao- lakini kumbuka tukianza kutumia video kuhakiki magoli mpira hautanoga tena. angalia goli la Teves lile ka kuotea, ni kweli aliotea lakini ile movement kabla ya yeye kumalizia lile goli ilikuwa classic kiasi cha kuwachangaya waamuzi - Tukichokonoa chokonoa sana tutaharibu uhondo wandugu.

Kwa wengi kutolewa kwa Uingeleza, Ufaransa na Italy ni misiba lakini bahati mbaya hizi timu hazikuwa na mpira wa kasi na dunia ya leo bila kasi na pasi za haraka haraka unapigwa tu.
Kwanza sijasema kutumia goal technology nimesema waongeze idadi ya waamuzi hasa kwenye goli kuondoa utata kwa makosa mengi yanayotokea ndani ya 18 ambayo ni ngumu sana linesman kuona
Mkubwa si sababu ya England hao walipaswa kufungwa hata 7 sababu timu yao ni mbovu.Angalia France walivyoqualify,Barca walibebwa against Chelsea.Haya mambo bora yatokee kwenye ligi na sio mashindano makubwa .Nawaonea huruma sana Mexico,US
 
Back
Top Bottom