Niliumia sana baad aya kuona nchi ya Tanzania imeshindwa kuonyesha hata mechi ya ufunguzi wa kombe la Afrika, hivi sisi kweli tunaweza nini? Kenya na Uganda wanaonyesha maana wanajua faida zake kuwa ni pamoja na kuwajengea vijana wetu hamu na morale ya kuipenda michezo, ni mahali pa kuitangaza Tanzania badala ya kutumia billions kwa kuweka matangazo CNN na TV za nje ambazo sioni wala siamini kama inasaidia lolote.Nilishangaa zaidi kukuta TBC2 ambayo kabla ya kuzinduliwa kipindi kile tuliambiwa itahusika na ishu kama hizi zaidi lakini badal a yake nikakuta KIDUKU, yaani kweli TBC nzima amekosekana mwenye akili hata mmoja ya ku-advice juu ya hili? Au kwasababu wana mkataba na hawa Wachin sasa wanataka watu wanunue Startimes? Hii haikubaliki, ni lazima tujifunze kutumia fursa kama hii kuwajengea vijana wetu uwezo wa kimawzo kuipenda michezo kama sehemu ya ajira. Jumapili Njema