ULAGHAI WA KIKWETE KUHUSU KUUNDWA KWA KATIBA YENYE WANANCHI KWENYE STERINGI SASA TUNASEMA BASI: TUNATAKA SERIKALI YA MPITO KUSHUGHULIKIA KATIBA NCHINI NA KUKAMILISHA KILA KITU 2014
CHADEMA,Asasi za Kiraia nchini, Vyuo Vikuu na Nchi Wahisani tunaomba mtuelewe kwamba sasa uzalendo umetushinda na huu utani wote na kiburi ya Mhe Kikwete - tunataka serikali mpya ya mpito sasa hivi kushughulikia katiba!!!
Wananchi; kila mmoja mahala ulipo wakati umefika wa kuachana na mchezo katika mambo ya msingi ambayo tumejaribu kutafuta kiungwana ndio hivo imeshindikana. Hakuna haja kuendelea kubisha mlango usiofunguliwa bali hapa ni kutafuta njia njingine kabisa kwa uwezo wa Nguvu ya Umma.
Cha msingi sasa sisi wenyewe tena vijana, kwa njia zetu zile, TUNAIPA SERIKALI YA Mhe Kikwete hadi April 08, 2011 iwe imewashirikisha wadau wote na mawazo yetu, katika hatua zote za ushiriki, usimamizi na uendeshaji wa mambo ya katiba kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na wala si kutulazimiza na matakwa ya watawala ambao ndio haswa tunaowalalamikia kwa unyanyasaji.
Vijana tuliowengi nchini tusimame kutetea haki zetu kwani haki hapewi mtu hata siku moja. Endpo serikali haitotii hayo maoni yetu basi Vijana kote nchini pamoja na taasisi marafiki wa UTAWALA WA KIDEMOKRASIA NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI MOJA KWA MOJA tujiweke tayari kwa maandamano ya amani kote nchini mpaka matakwa haya yatimizwe au serikali inaposhindwa basi ikatupishe njia haraka!!
Tunasema katika huu mzaha wa serikali kuhusu tume HURU YA BUNGE kugeuzwa kuwa TUME TEGEMEZI YA RAIS ikibarikiwa na Bunge; Vijana tumefika Tamati tena hadi hapa!!!
Kumbe Kupatikana kwa Katiba Mpya chini ya Uongozi wa CCM haiwezikani bila serikali kututwisha MADALALI kwenye mambo ya kuundwa kwa Katiba Mpya nchini.
CHADEMA tusikilizeni, tunahitaji kwana SERIKALI YA MPITO kumbe yenye jukumu moja tu kushughulikia Katiba kwa MUJIBU WA MATAKWA WA WANANCHI katika hatua zote za usimamizi na maamuzi.
BAVICHA na matawi yetu yote ya CHADEMA nchini tueleweni kwamba wananchi sasa tunasema baaasi na Serikali ya CCM iondoke madarakani sasa hivi. Sote tunao uwezo wa kubadilisha haya mambo yote kabla hatujaingizwa porini zaidi.
Mwenye kupata ujumbe huu na akawajulishe vijana wengine 10 juu ya ulaghai uliotangazwa na serikali majuzi kutupora haki ya kusimamia kuundwa kwa katiba mpya bila kuingiliwa na dola.
Lengo lao likiwa ni kuleta katiba waitakayo MAFISADI nchini, kuchelewesha muda tuingie uchaguzi 2015 bila katiba mpya, na vile vile kukiundia CHADEMA mikesi ya kuchonga kisiasa ili baadhi ya wale tunaowapenda wasigombee.
SASA TUNASEMA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI BARA NA VISIWANI YOTE YAWEZEKANA BILA CCM, TUPISHENI NJIA!!!